MASOMO
YA MISA, NOVEMBA 9, 2021
JUMANNE,
JUMA LA 32 LA MWAKA
SIKUKUU
KUTABARUKIWA BASILIKA LA LATERANI
---------------
SOMO
1
Eze.
43:1-2, 4-7
Malaika
alinileta mpaka langoni, yaani, lango lile lielekealo upande wa mashariki; na
tazama, huo utukufu wa Mungu wa Israeli ulitokea kwa njia ya mashariki; na
sauti yake ilikuwa kama mshindo wa maji mengi, nayo nchi iling’aa kwa utukufu
wake. Na huo utukufu wa Bwana ukaingia ndani ya nyumba, kwa njia ya lango lile
lielekealo upande wa mashariki. Kisha Roho ikaniinua, ikanichukua mpaka ua wa
ndani; na tazama, utukufu wa Bwana uliijaza nyumba. Nikasikia sauti ya mmoja
asemaye nami, itokayo katika nyumba hiyo; na mtu akasimama karibu nami.
Akaniambia, Mwanadamu, hapa ni mahali pa kiti changu cha enzi, na mahali pa
nyayo za miguu yangu, nitakapokaa kati ya wana wa Israeli milele.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
------------
SOMO
2
1Kor.
3:9-11, 16-17
Ninyi
ni jingo la Mungu. Kwa kadiri ya neema ya Mungu niliyopewa, mimi, kama mkuu wa
wajenzi mwenye hekima, naliuweka msingi, na mtu mwingine anajenga juu yake.
Lakini kila mtu na aangalie jinsi anavyojenga juu yake. Maana msingi mwingine
hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani, yesu
Kristo. Lakini kama mtu akijenga juu ya msingi huo, dhahabu au fedha au mawe ya
thamani, au miti au majani, au manyasi, kazi ya kila mtu itakuwa Dhahiri. Maana
siku ile itaidhihirisha, kwa kuwa yafunuliwa katika moto; na ule moto wenyewe
utaijaribu kazi ya kila mtu, ni ya namna gani.
Hamjui
ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, nay a kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani
yenu? Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa
maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
--------------------
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
95:1-7 (K)
(K)
Tuje mbele za Bwana kwa shukrani.
Njoni,
tumwimbie Bwana,
Tumfanyie
shangwe mwamba wa wokovu wetu.
Tuje
mbele zake kwa shukrani,
Tumfanyie
shangwe kwa zaburi. (K)
Kwa
kuwa Bwana ni Mungu mkuu,
Na
mfalme mkuu juu ya miungu yote.
Mkononi
mwake zimo bonde za dunia,
Hata
vilele vya milima ni vyake.
Bahari
ni yake, ndiye aliyeifanya,
Na
mikono yake iliiumba nchi kavu. (K)
Njoni,
tuabudu, tusujudu,
Tupige
magoti mbele za Bwana aliyetuumba.
Kwa
maana ndiye Mungu wetu,
Na
sisi tu watu wa malisho yake,
Na
kondoo za mkono wake. (K)
----------------
SHANGILIO
2
Nya. 7:16
Aleluya,
aleluya,
Nimeichagua
nyumba hii na kuitakasa, asema Bwana, ili kwamba jina langu lipate kuwako huko
milele.
Aleluya.
-------------------------
INJILI
Yn.
2: 13-22
Pasaka
ya Wayahudi ilikuwa karibu; naye Yesu alikwea mpaka Yerusalemu. Akaona pale
hekaluni watu waliokuwa wakiuza ng’ombe na kondoo na njiwa, na wenye kuvunja
fedha wameketi. Akafanya kikoto cha kambaa, akawatoa wote katika hekalu, na
kondoo na ng’ombe; akamwaga fedha za wenye kuvunja fedha, akazipindua meza zao;
akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, Yaondoeni haya; msiifanye nyumba ya
Baba yangu kuwa nyumba ya biashara. Wanafunzi wake wakakumbuka ya kuwa
imeandikwa, Wivu wa nyumba yako utanila.
Basi
Wayahudi wakajibu, wakamwambia, Ni ishara gani utuonyeshayo, kwamba unafanya
haya? Yesu akajibu, akawaambia, Livunjeni hekalu hili, name katika siku tatu
nitalisimamisha. Basi Wayahudi wakasema, Hekalu hili lilijengwa katika muda wa
miaka arobaini na sita, nawe utalisimamisha katika siku tatu? Lakini yeye
alinena habari za hekalu la mwili wake. Basi alipofufuka katika wafu, wanafunzi
wake wakakumbuka ya kuwa alisema hivi, wakaliamini lile andiko na lile neno
alilolinena Yesu.
Neno
la Bwana... Sifa kwako Ee Kristo
Copyright © 2020, "MASOMO YA
MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings
reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment