ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya kila siku
Jumatatu,
Oktoba4, 2021,
Juma
la 27 la Mwaka
Yon
1: 1,2:1-10
Lk
10: 25-37.
Karibuni ndugu zangu kwa adhimisho la
Ekaristi asubuhi ya leo. Leo ni kumbukumbu ya Maria Mama wa Rozari. Neno la
Bwana tunaanza kwa kuliangalia somo la kwanza linatoka katika kitabu cha
Matendo ya Mitume. Hapa tunakumbana na habari ya Mama Maria akiwa amejiunga
pamoja na kundi la mitume akisali-wakiwa katika maombi makubwa.
Walikuwa katika maombi makubwa kwa
sababu walikuwa hawako na Bwana Yesu. Bwana Harusi alikuwa amekwisha ondolewa.
Hivyo walikuwa wanajitahidi kusali kwa nguvu sana ili Mungu asi awaache, ili
shetani asije akawashinda kwa sababu Bwana harusi wa kuwatetea hayupo tena kati
yao.
Tunapokuja katika injili ya leo,
tunakumbana na somo machachari kabisa. Hapa tunakutana na simulizi la kupashwa
habari Maria. Katika simulizi hili, Maria anatajwa kwamba amejaa neema, na
Bwana yupo naye kila wakati, na yeye ni mbarikiwa kuliko wanawake wote na hata
kile atakachokizaa kimebarikiwa. Hapa tunaona juu ya huu ukuu wa Maria.
Lakini unaporudi tena katika somo la
kwanza, unaona kwamba licha ya huyu Mama kuwa na cheo kikubwa, zaidi kuliko
hata mitume na wanawake wenzake-yeye bado ni mnyenyekevu, bado anabakia katika
sala, yeye anawatia moyo wale wanawake na mitume waliokuwa katika kukata tamaa,
yeye anakuwa kwao mfano wa utii, unyenyekevu na unyofu. Anaona cheo chake kama
sehemu ya huduma na si kujipatia utukufu Zaidi. Anatumia cheo chake kuwavuta
watu kwa Mungu zaidi.
Tabia ya namna hii ndugu zangu ndiyo
iliyompatia Mama Maria hata cheo cha kuwa mwombzi, mwombezi wa wanadamu kwa
Kristo, kwani ni Mama aliyeungana kikamilifu na wanadamu. Pia ameungana na
Mungu sawa sawa.
Ndugu zangu, hapa tunayomengi ya
kujifunza: kwanza kati yetu wapo waliobarikiwa na Mungu, wamejazwa neema
mbalimbali na Mungu: wewe unazitumiaga je? Unawafanyaga watu wamjue Mungu
zaidi, Mungu atukuke zaidi kupitia kwako au unatumiaga hizo neema za Mungu
kujitangaza? Nakwambia kati yetu tumezidi kutumia neema za Mungu kugandamiza
wenzetu, kuwaengezea shida, kufurahisha vionjo vyetu-unakuta wewe ni mwalimu
chuoni unamwambia mwanafunzi usipotoa kitu, basi nitakufelisha! ndugu yangu!
Unakuta mtu umebarikiwa kuwa na kampuni
yako lakini kila mwanadada atakayeomba kazi kwako lazima alale nawe-nakwambia
huku ni kuchezea neema za Mungu ndugu yangu na anayefanya hivyo nakwambia tubu
mapema kwa sababu mambo yatakuwia mabaya sana siku moja
Neema alizokujalia Mwenyezi Mungu
zifanye ziwawezeshe wengine wamjue Mungu-yaani vipaji na uwezo uliojaliwa na
Mungu vimtangaze Mungu na si kumtangaza shetani. Hivi vipaji ni vya Mungu na si
vya shetani. usikubali shetani atukuke katika hivi vipaji.
Mama Maria alijiunga na mitume ili
kuwapa moyo na pia kuwafundisha kusali. Sisi nasi kama watu tuliobarikiwa na
Mungu na kujawa neema, tusiwakwaze wenzetu bali waongoze wote kwa Kristo.
Ameni.
Copyright ©2013-2021 ©FurKat,
Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment