MASOMO YA MISA, OKTOBA 15, 2025
JUMATANO, JUMA LA 28 LA MWAKA
JUMATANO, JUMA LA 28 LA MWAKA
KUMBUKUMBU YA MTAKATIFU TERESIA WA AVILA
SOMO 1
Rum. 2:1-11
Wewe mtu uwaye yote uhukumuye, huna udhuru; kwa maana katika hayo umhukumuyo mwingine wajihukumu mwenyewe kuwa na hatia; kwa maana wewe uhukumuye unafanya yale yale. Nasi twajua ya kuwa hukumu ya Mungu ni ya kweli juu yao wafanyao hayo. Wee binadamu, uwahukumuye wale wafanyao hayo na kutenda yayohayo mwenyewe, je! Wadhani ya kwamba utajiepusha na hukumu ya Mungu? Au waudharau wingi wa wema wake na ustahimili wake na uvumilivu wake, usijue ya kuwa wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu? Bali kwa kadiri ya ugumu wako, na kwa moyo wako usio na toba, wajiwekea akiba ya hasira kwa siku ile ya hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu, atakayemlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake; wale ambao kwa saburi katika kutenda mema wanatafuta utukufu na heshima na kutokuharibika, watapewa uzima wa milele; na wale wenye fitina, wasiiotii kweli, bali wakubalio dhuluma, watapata hasira na ghadhabu; dhiki na shida juu ya kila nafsi ya mwanadamu atendaye uovu, Myahudi kwanza na Myunani pia; bali utukufu na heshima na Amani kwa kila mtu atendaye mema, Myahudi kwanza na Myunani pia; kwa maana hakuna upendeleo kwa Mungu.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 62:1-2.5-6.8 (K) 12
(K) Bwana humlipa kila mtu sawasawa na haki yake.
Nafsi yangu yamngoja Mungu peke yake kwa kimya,
Wokovu wangu hutoka kwake.
Yeye tu ndiye mwamba wangu na wokovu wangu,
Ngome yangu, sitatikisika sana. (K)
Nafsi yangu, umngoje Mungu peke yake kwa kimya,
Tumaini langu hutoka kwake.
Yeye tu ndiye mwamba wangu na wokovu wangu,
Ngome yangu, sitatikisika sana. (K)
Enyi watu, mtumaini siku zote,
Ifunueni mioyo yenu mbele zake;
Mungu ndiye kimbilio letu. (K)
SHANGILIO
Zab. 27:11
Aleluya, aleluya,
Ee Bwana, unifundishe njia yako, na kuniongoza katika njia iliyonyoka.
Aleluya.
INJILI
Lk. 11:42-46
Yesu aliwaambia Mafarisayo: Ole wenu, Mafarisayo, kwa kuwa mwatoa zaka za mnanaa na mchicha na kila mboga, na huku mwaacha mambo ya adili, na upendo wa Mungu; iliwapasa kuyafanya hayo ya kwanza, bila kuyaacha hayo ya pili. Ole wenu, Mafarisayo, kwa kuwa mwapenda kuketi mbele katika masinagogi, na kusalimiwa masokoni. Ole wenu, kwa kuwa mmefanana na makaburi yasiyoonekana, ambayo watu wapitao juu yake hawana habari nayo.
Mtu mmoja katika wanasheria akajibu, akamwambia, Mwalimu, kwa kusema hayo umetushutumu sisi nasi. Akasema, Nanyi wanasheria, ole wenu, kwa sababu mwawatwika watu mizigo isiyochukulika, wala ninyi wenyewe hamwigusi mizigo hiyo hata kwa kimoja cha vidole vyenu.
Neno la Bwana...Sifa kwako, Ee Kristo
Copyright © 2025, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment