“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Jumatano, Oktoba 15,
2025,
Juma la 28 la Mwaka wa
Kanisa
Rom 2: 1-11;
Lk 11: 42-46.
KUJIZOESHA KUTENDA
FADHILA!
Yesu anawataja walimu
washeria na Mafarisayo kwa maneno makali kabisa. Yesu anatumia mfano wa zaka
kuonesha ni kwa jinsi ghani walivyotoka njee ya mstari. Mungu alitaka sadaka ya
mazao ya kwanza kama shukrani na heshima ya nguvu zake kwa kujali watu wake
(Kumb. 14: 22; Lev. 27: 30).
Waandishi walienda
mbali zaidi na kuwatoza watu zaidi tena kwa kutumia mahesabu na ujazo usio wa
muhimu, na kushindwa kuwajali maskini na wahitaji. Walishikwa na wivu na
kushindwa kuwapenda wengine. Yesu pia anawalinganisha pia na “makaburi yasio na
mipaka” ilikuwa mtu akijigusa na kaburi alikuwa anatiwa najisi kwa muda wa siku
saba (Hes 19:16). Wale wote waliokuja kuwasikiliza Mafarisayo na waandishi kadhalika
walitiwa unajisi kwa mafundisho yao ya uongo.
Kiini cha amri za
Mungu ni upendo. Mungu ni Upendo na kila kitu anchotenda kinatoka katika upendo
wake kwetu sisi. Je, una ruhusu Upendo wa Mungu ubadili akili yako na moyo
wako? Je, upo tayari kukuwa katika fadhila katika upendo kwa Mungu na jirani?
Fadhila inapaswa kupaliliwa kwa sala na matendo mema ili zikuwe na zimee ndani
kabisa mwa mioyo yetu, ili ziweze kukomaa na kuchanua. Kama vile mimea inavyo
hitaji maji na mbolea ili imee vizuri, ndivyo na fadhila za Kimungu zinapaswa
kumwagiliwa kwa kuzitenda kila wakati na kuwa karibu zaidi na Mungu. Tumuombe Mungu atusaidie kusogea karibu naye
daima, kadiri unavyokuwa karibu na taa ndivyo uhakika wakuona unakuwepo.
usaidie kusogea karibu naye daima, kadiri unavyokuwa karibu na taa ndivyo
uhakika wakuona unakuwepo. Tuishi kama Mungu anavyopenda ili tutende kwa upendo
kama Mungu anavyotutendea.
Sala: Bwana, washa
ndani ya moyo wangu kwa upendo ili niweze kutenda yale yalio ya lazima
kabisa-Upendo kwa Mungu na Upendo kwa Jirani. Amina.
Copyright ©2013-2025 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com
No comments:
Post a Comment