MASOMO
YA MISA OCTOBER 2, 2021
JUMAMOSI,
JUMA LA 26 LA MWAKA
WATAKATIFU
MALAIKA WALINZI
SOMO
1
Kut.
23:20-23
Bwana
asema hivi: Tazama, mimi namtuma malaika aende mbele yako, ili akulinde njiani
na kukupeleka mpaka mahali pale nilipokutengezea. Jitunzeni mbele yake,
mwisikize sauti yake; wala msimtie kasirani; maana, hatawasamehe makossa yenu;
kwa kuwa jina langu limo ndani yake. Lakini ukiisikiza sauti yake kweli, na
kuyatenda yote ninenayo mimi; ndipo mimi nitakuwa ni adui wa adui zako, na
mtesi wa hao wakutesao. Kwa kuwa malaika wangu atatangulia mbele yako, na
kukufikisha kwenye Mwamori, na Mhiti, na Mpezi, na Mkanaani, na Mhivi, na
Myebusi; name nitawakatilia mbali.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
91:1-6.10-11
(K)
Amekuagizia malaika zake wakulinde katika njia zako zote.
Aketiye
mahali pa siri pake aliye juu,
Atakaa
katika uvuli wake Mwenyezi.
Nitasema,
Bwana ndiye kimbilio langu na ngome yangu,
Mungu
wangu nitakayemtumaini. (K)
Maana
Yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji,
Na
katika tauni iharibuyo.
Kwa
manyoya yake atakufunika,
Chini
ya mbawa zake utapata kimbilio. (K)
Hutaogopa
hofu ya usiku,
Wala
mshale urukao mchana,
Wala
tauni ipitayo gizani.
Wala
uele uharibuo adhuhuri, (K)
Mabaya
hayatakupata wewe,
Wala
tauni haitaikaribia hema yako.
Kwa
kuwa atakuagizia malaika zake
Wakulinde
katika njia zako zote. (K)
SHANGILIO
Mt.
18:1-5,10
Aleluya,
aleluya,
Mhimidini
Bwana, enyi majeshi yake yote, ninyi watumishi wake mfanyao mapenzi yake.
Aleluya.
INJILI
Mt.
18:1-5.10
Wanafunzi
walimwendea Yesu wakisema, Ni nani basi aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni?
Akaita mtoto mmoja, akamweka katikati yao, akasema, Amin, nawaambia,
Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.
Basi, yeyote ajinyenyekeshaye mwenyewe kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu
katika ufalme wa mbinguni.
Na
yeyote atakayempokea mtoto mmoja mfano wa huyu kwa jina langu, anipokea mimi.
Angalieni
msidharau mmojawapo wadogo hawa; kwa maana nawaambia ya kwamba malaika zao
mbinguni sikuzote huutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
-------------------------
Copyright © 2020,
"MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora –
Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment