“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya kila siku
Alhamisi,
Septemba 30, 2021.
Juma
la 26 la Mwaka
Neh
8: 1-12;
Zab
18:8-11;
Lk
10: 1-12
UFUASI
MAANA YAKE UTUME
Karibuni
sana wapendwa wa Mungu kwa adhimisho la misa takatifu asubuhi ya leo. Neno la
Bwana katika somo la kwanza Ezra anaisoma sheria ya Bwana, kitabu kitakatifu
machoni pa wana wa Yuda waliorudi utumwani. Walipokuwa utumwani, walikosa
Torati takatifu ya Musa. Hawakuwa na mtu wa kuwasomea, walisikiliza tu habari
za miungu ya kipagani, na miziki ya kipagani, na hivyo mioyo yao ilikuwa tupu
sana. Mioyo yao ilitamani ilishwe na neno la Mungu, na kupewa matumaini. Na leo
wanaonesha kwamba yapo matumaini makubwa, ipo lishe kubwa katika neno la Mungu,
yaani Biblia.
Hivyo
wanapopatiwa lishe hii siku ya leo, wanafurahi na kuburudika.
Sisi
tujifunze kulisoma neno la Mungu, hakika litatupatia maarifa, litatuonya na
kutupatia maarifa. Wengi wetu tunakosa maarifa mengi kwa sababu hatusomi
maandiko matakatifu. Kila tukijisikia kukosa matumaini, tujisikia hofu na
ukosefu wa tumaini ni vyema kuyakimbilia maandiko matakatifu. Hakika tutapata
maarifa na matumaini.
Hakika
wengi kati yetu hatuna maarifa, tunayumbishwa na ushirikina, tamaa za kimwili,
kwa sababu hatuyajui vyema maandiko matakatifu. Pia turuhusu neno la Mungu
lituchome na kutuumbua. Ni kwa sababu neno la Mungu limebeba roho yenye uwezo
wa kutugeuza, na kutufanya tuwe huru zaidi. Tusiache kusoma maandiko
matakatifu.
Katika
somo la injili, Bwana Yesu anawatuma wafuasi wake wakahubiri injili. Anafanya
hivi kwani dunia inahitaji iletewe ukombozi na injili. Bila injili, dunia
itatetereka tu. Injili ndiyo itakayoleta amani duniani, kuheshimiana,
kupendana, na kufurahiana. Sisi tukubali tuwe wafuasi wa kuitangaza injili.
Tukubali kutumwa.
Mara
nyingi tunamkweza na kumtangaza shetani kuliko injili. Shetani anaonekana kuwa
na nguvu zaidi kuliko injili yenyewe. Tuipende injili na hakika tutajiletea
ukombozi zaidi ndani ya maisha yetu na kuishi kwa ubora zaidi. Tuipende injili
kwa siku zote. Tusiiache pembeni injili ya Bwana.
------------------------
Copyright ©2013-2020
©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment