MASOMO
YA MISA, SEPTEMBA 30, 2021,
ALHAMISI
JUMA 26 LA MWAKA
________
SOMO
1
Neh.
8:1-12
Watu
wote walikusanyika kama mtu mmoja katika uwanja uliokuwa mbele ya lango la
maji; wakamwambia Ezra, mwandishi, akilete kitabu cha torati ya Musa, Bwana
aliyowaamuru Israeli. Naye Ezra, kuhani, akaileta torati mbele ya kusanyiko, la
wanaume na wanawake, na wote walioweza kusikia na kufahamu, siku ya kwanza ya
mwezi wa saba. Akasoma humo mbele ya uwanja uliokuwa ukikabili lango la maji,
tangu mapambazuko hata adhuhuri, mbele ya hao wanaume na wanawake, na wale
walioweza kufahamu; na masikio ya watu wote yakasikiliza kitabu cha torati.
Naye
Ezra, kuhani, akasimama kwa kusudi hilo; na karibu naye wakasimama, Matithia,
na Shema, na Anaya, na Uria, na Hilkia, na Maaseya, mkono wake wa kuume; na
mkono wake wa kushoto, Pedaya, na Mishaeli, na Milkiya, na Hashumu, na
Hashbadani, na Zekaria, na Meshulamu. Ezra akakifungua kitabu machoni pa watu
wote; (maana alikuwa juu ya watu wote); na hapo alipokifungua, watu wote
walisimama; Ezra akamhimidi Bwana, Mungu Mkuu. Nao watu wote wakaitika, Amina,
Amina, pamoja na kuinua mikono yao; kisha wakainama vichwa vyao, wakamsujudu
Bwana kifudifudi.
Walawi,
wakawafahamisha watu torati; na watu wakasimama mahali pao. Nao wakasoma katika
kitabu, katika torati ya Mungu, kwa sauti ya kusikilika; wakaeleza maana yake,
hata wakayafahamu yaliyosomwa.
Naye
Nehemia, ndiye aliyekuwa Tirshatha, na Ezra kuhani, mwandishi, na Walawi
waliowafundisha watu, wakawaambia watu wote, Siku hii ni takatifu kwa Bwana,
Mungu wenu; msiomboleze wala msilie. Maana watu wote walilia, walipoyasikia
maneno ya torati.
Kisha
akawaambia, Enendeni zenu, mle kilichonona, na kunywa kilicho kitamu, tena
mpelekeeni sehemu yeye asiyewekewa kitu; maana siku hii ni takatifu kwa Bwana
wetu; wala msihuzunike; kwa kuwa furaha ya Bwana ni nguvu zenu. Hivyo Walawi
wakawatuliza watu wote, wakasema, Nyamazeni, kwa maana siku hii ni takatifu;
wala msihuzunike. Na watu wote wakaenda zao kula na kunywa, na kuwapelekea watu
sehemu, na kufanya furaha nyingi, kwa sababu walikuwa wameyafahamu maneno yale
waliyohubiriwa.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
________
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
19:7-10 (K) 8
(K)
Amri ya Bwana huufurahisha moyo
Sheria
ya Bwana ni kamilifu,
Huiburudisha
nafsi.
Ushuhuda
wa Bwana ni amini,
Humtia
mjinga hekima. (K)
Maagizo
ya Bwana ni ya adili,
Huufurahisha
moyo.
Amri
ya Bwana ni safi,
Huyatia
macho nuru. (K)
Kicho
cha Bwana ni kitakatifu,
Kinadumu
milele.
Hukumu
za Bwana ni kweli,
Zina
haki kabisa. (K)
Ni
za kutamanika kuliko dhahabu,
Kuliko
wingi wa dhahabu safi.
Nazo
ni tamu kuliko asali,
Kuliko
sega la asali. (K)
________
SHANGILIO
Mt.
11:25
Aleluya,
aleluya,
Nakushukuru,
Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na
akili, ukawafunulia watoto wachanga.
Aleluya.
________
INJILI
Lk.
10:1-12
Bwana
aliweka wafuasi wengine, sabini na wawili wamtangulie kwenda kila mji na kila
mahali alipokusudia kwenda mwenyewe. Akawaambia, Mavuno ni mengi, lakini
watenda kazi ni wachache; basi mwombeni Bwana wa mavuno apelike watenda kazi
katika mavuno yake. Enendeni; angalieni, nawatuma kama wana-kondoo kati ya
mbwa-mwitu. Msichukue mfuko, wala mkoba, wala viatu; wala msimwamkie mtu
njiani.
Na
nyumba yoyote mtakayoingia, semeni kwanza, Amani iwemo nyumbani humu; na
akiwamo mwana wa Amani, Amani yenu itamkalia; la, hayumo, Amani yenu itarudi
kwenu. Basi, kaeni katika nyumba iyo hiyo, mkila na kunywa vya kwao; maana,
mtenda kazi amestahili kupewa ujira wake. Msihame-hame kutoka nyumba hii kwenda
nyumba hii. Na mji wowote mtakaouingia, wakiwakaribisha, vileni vyakula
viwekwavyo mbele yenu; wapozeni wagonjwa waliomo, waambieni, Ufalme wa Mungu
umewakaribia.
Na
mji wowote mtakaouingia, nao hawawakaribishi, tokeni humo, nanyi mkipita katika
njia zake semeni, Hata mavumbi ya mji wenu yaliyogandamana na miguu yetu
tunayakung’uta juu yenu. Lakini jueni hili, ya kuwa Ufalme wa Mungu umekaribia.
Nawaambia ya kwamba siku ile itakuwa rahisi Zaidi Sodoma kuistahimili adhabu
yake kuliko mji huo.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
-------------------------
Copyright © 2020,
"MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora –
Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment