MASOMO
YA MISA, SPTEMBA 28, 2021
JUMANNE,
JUMA LA 26 LA MWAKA
SOMO
1
Zek.
8:20-23
Bwana
wa majeshi asema hivi, Itatokea halafu ya kwamba watakuja mataifa na wenyeji wa
miji mingi; wenyeji wa mji huu watauendea mji huu, wakisema, Haya! Twendeni
zetu kwa haraka tuombe fadhili za Bwana, na kumtafuta Bwana wa majeshi; Mimi
nami nitakwenda. Naam, watu wa kabila nyingi na mataifa hodari watakuja
Yerusalemu kumtafuta Bwana wa majeshi, na kuomba fadhili za Bwana.
Bwana
wa majeshi asema hivi, Siku hizo watu kumi, wa lugha zote za mataifa,
wataushika upindo wa nguo yake yeye aliye Myahudi; naam, wataushika wakisema,
Tutakwenda pamoja nanyi, kwa maana tumesikia kwamba Mungu yu pamoja nanyi.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
87 (K) Zek. 8:23
(K)
Mungu yu pamoja nasi.
Msingi
wake upo
Juu
ya milima mitakatifu.
Bwana
ayapenda malango ya Sayuni
Kuliko
maskani zote za Yakobo.
Umetajwa
kwa mambo matukufu,
Ee
Mji wa Mungu. (K)
Nitataja
Rahabu na Babeli
Miongoni
mwao wanaonijua.
Tazama
Filisti, na Tiro, na Kushi;
Huyu
alizaliwa humo.
Naam,
mintarafu Sayuni itasemwa,
Huyu
na huyu alizaliwa humo. (K)
Na
Yeye Aliye juu
Ataufanya
imara.
Bwana
atahesabu, awaandikapo mataifa,
Huyu
alizaliwa humo.
Waimbao
na wachezao na waseme,
Visiwa
vyangu vyote vimo mwako. (K)
SHANGILIO
Zab.
119:105
Aleluya,
Aleluya,
Neno
lako ni taa ya miguu yangu, na mwanga wa njia yangu.
Aleluya.
INJILI
Lk.
9:51 – 56
Ilikuwa,
siku za kupaa kwake zilipokuwa karibu kutimia, Yesu aliukaza uso wake kwenda
Yerusalemu; akatuma wajumbe kutangulia mbele ya uso wake; wakaenda wakaingia
katika kijiji cha Wasamaria, ili kumtengenezea mahali. Lakini wenyeji
hawakumkaribisha kwa vile alivyouelekeza uso wake kwenda Yerusalemu. Wanafunzi
wake Yakobo na Yohane walipoona hayo, walisema, Bwana, wataka tuagize moto
ushuke kutoka mbinguni, uwaangamize? Akawageukia akawakanya, wakaondoka
wakaenda mpaka kijiji kingine.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
-------------------------
Copyright © 2020,
"MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora –
Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment