Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

MASOMO YA MISA SEPTEMBA 25, 2021

 

MASOMO YA MISA SEPTEMBA 25,  2021

JUMAMOSI, JUMA LA 25 LA MWAKA

 

SOMO I

Zek. 2:1-5, 10-11

 

Niliinua macho yangu, nikaona, na atazama, mtu mwenye Kamba ya kupimia mkononi mwake. Ndipo nikasema, Unakwenda wapi? Akaniambia, Ninakwenda kuupima Yerusalemu, nione upana wake ulivyo na urefu wake ulivyo. Na tazama, yule malaika aliyesema nami akasimama karibu, na malaika mwingine akatoka ili kuonana naye; naye akamwambia, Piga mbio, kamwambie kijana huyu, na kusema, Yerusalemu utakaliwa na watu, kama vijiji visivyo na kuta, kwa sababu ya wingi wa watu na mifugo iliyomo ndani yake. Kwa maana mimi, asema Bwana, nitakuwa ukuta wa moto kuuzunguka pande zote, nami nitakuwa huo utufukuf ndani yake.

Imba, ufurahi, Ee binti Sayuni; maana, tazama, ninakuja, nami nitakaa, kati yako, asema Bwana. Na mataifa mengi watajiunga na Bwana katika siku ile, nao watakuwa watu wangu.

 

Neno la Mungu… Tumshukuru Bwana.

 

WIMBO WA KATIKATI

Yer. 31:10-13 (K) 10

 

(K) Bwana atatulinda kama mchungaji alindavyo kundi lake.

 

Lisikieni neno la bwana, enyi mataifa,

Litangazeni visiwani mbali,

Mkaseme, aliyemtawanya Israeli atamkusanya,

Na kulinda kama mchungaji alindavyo kundi lake. (K)

 

Kwa maana Bwana amemweka huru Yakobo,\

Amemkomboa mkononi mwake

Aliyekuwa hodari kuliko yeye.

Nao watakuja, na kuimba katika mlima Sayuni,

Wataukimbilia wema wa Bwana. (K)

 

Ndipo bikira atafurahi katika kucheza,

Na vijana na wazee pamoja,

Maana nitageuza masikitiko yao kuwa furaha,

Nami nitawafariji,

Na kuwafurahisha waache huzuni zao. (K)

 

SHANGILIO

Zab. 19:8

 

Aleluya, aleluya,

Amri ya Bwana ni safi, huyati amacho nuru.

Aleluya.

 

INJILI

Yn. 1:47-51

 

Yesu alipomwona Nathanaeli anakuja kwake akanena habari zake, Tazama, Mwisraeli kweli kweli, hamna hila ndani yake. Nathanaeli akamwambia, Umepataje kunitambua? Yesu akajibu, akamwambia, Kabla Filipo hajakuita, ulipokuwa chini ya mtini nilikuona. Nathanaeli akamjibu, Rabi, wewe u Mwana wa Mungu, ndiwe Mfalme wa Israeli. Yesu akajibu, akamwambia, kwa sababu nilikuambia, Nilikuona chini ya mtini, waamini? Utaona mambo makubwa kuliko haya. Akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Mtaziona mbingu zimefunguka na malaika wa Mungu wakikwea na kushuka juu ya Mwana wa Adamu.

 

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.

 

-------------------------

Copyright © 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.

No comments:

Post a Comment