MASOMO YA MISA, SEPTEMBA 23, 2021
ALHAMISI,
JUMA LA 25 LA MWAKA
SOMO
1
Hag.
1:1-8
Katika
mwaka wa pili wa Dario mfalme, mwezi wa sita, siku ya kwanza ya mwezi, neno la
Bwana lilimjia Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, liwali wa Yuda na Yoshua, mwana
wa Yeosadaki, kuhani mkuu, kwa kinywa chake Hagai nabii, kusema, Bwana wa
majeshi asema hivi, ya kwamba, watu hawa husema, hu sio wakati utupasao kuja,
huu sio wakati wa kujengwa nyumba ya Bwana. Ndipo neno la Bwana lilikuja kwa
kinywa cha nabii Hagai, kusema, Je! Huu ndio wakati wa ninyi kukaa katika
nyumba zenye mapambo ya mbao, iwapo nyumba hii inakaa hali ya kuharibika? Basi
sasa. Bwana wa majeshi asema hivi, Zitafakarini njia zenu. Mmepanda mbegu
nyingi mkavuna kidogo; mnakula lakini hamshibi; mnakunywa lakini hamkujazwa na
vinywaji; mnajivika nguo lakini hapana aonaye moto; nay eye apataye mshahara
apata mshahara ili kuutia katika mfuko uliotoboka. Bwana wa majeshi asema hivi,
Zitafakarini njia zenu. Pandeni milimani, mkalete miti, mkaijenge nyumba; nami
nitaifurahia, nami nitatukuzwa, asema Bwana.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
________
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
149:1-6, 9 (K) 4
(K)
Bwana awaridhia watu wake.
Aleluya,
Mwimbieni
Bwana wimbo mpya,
Sifa
zake katika kusanyiko la watauwa!
Israeli
na amfurahie Yeye aliyemfanya,
Wana
wa Sayuni na wamshangilie mfalme wao! (K)
Na
walisifu jina lake kwa kucheza,
Kwa
matari na kinubi wamwimbie!
Kwa
kuwa Bwana awaridhia watu wake,
Huwapamba
wenye upole kwa wokovu. (K)
Watauwa
na waushangilie utukufu,
Waimbe
kwa sauti kuu vitandani mwao.
Sifa
kuu za Mungu na ziwe vinywani mwao,
Na
upanga mkali kuwili mikononi mwao. (K)
Kuwafanyia
hukumu iliyoandikwa:
Hiyo
ndiyo heshima ya watauwa wake wote. (K)
________
SHANGILIO
Zab.
27:11
Aleluya,
aleluya,
Ee
Bwana, unifundishe njia yako, na kuniongoza katika njia iliyonyoka.
Aleluya.
________
INJILI
Lk.
9:7 – 9
Herode
mfalme alisikia habari za yote yaliyotendeka, akafadhaika kwa sababu watu
wengine walisema ya kwamba Yohane amefufuka katika wafu, na wengine ya kwamba
Eliya ametokea, na wengine ya kwamba mmojawapo wa manabii wa kale amefufuka.
Lakini Herode akasema, Yohane nilimkata kichwa; basi ni nani huyu ambaye
ninasikia mambo haya juu yake? Akataka kumwona.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo
-------------------------
No comments:
Post a Comment