MASOMO
YA MISA, SEPTEMBA 22, 2021
JUMATANO,
JUMA LA 25 LA MWAKA
SOMO
1
Ezr.
9:5-9
Wakati
wa sadaka ya jioni, mimi Ezra niliinuka baada ya kunyenyekea kwangu, nguo yangu
na joho yangu zimeraruliwa, nikaanguka magotini nikakunjua mikono yangu mbele
za Bwana, Mungu wangu; nikasema, Ee Mungu wangu, nimetahayari, naona haya
kuinua uso wangu mbele zako, Mungu wangu; kwa maana maovu yetu ni mengi, hata
yamefika juu ya vichwa vyetu, na hatia yetu imeongezeka na kufika mbinguni.
Tangu siku za baba zetu tumekuwa na hatia kupita kiasi hata leo; na kwa sababu
ya maovu yetu sisi, na wafalme wetu, na makuhani wetu, tumetiwa katika mikono
ya wafalme wa nchi hizi, tumepigwa kwa upanga, tumechukuliwa mateka,
tumenyang’anywa mali zetu, tumetiwa haya nyuso zetu, kama hivi leo. Na sasa kwa
muda kidogo tumeneemeshwa na Bwana, Mungu wetu, hata akatuachia mabaki yaokoke,
akatupa msumari katika mahali pake patakatifu. Mungu wetu atutie nuru machoni
mwetu, tuburudike kidogo katika kufungwa kwetu. Maana sisi tu watumwa; lakini
Mungu wetu hakutuacha katika utumwa wetu, bali ametufikilizia rehema zake,
mbele ya wafalme wa Uajemi, ili kutuburudisha, tuisimamishe nyumba ya Mungu
wetu, na kuitengeneza palipobomoka, atupe ukuta katika Yuda na Yerusalemu.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
________
WIMBO
WA KATIKATI
Tob.
13:2-4, 6 (K) 1
(K)
Amehimidiwa Mungu aishiye milele.
Kwa
maana hurudi, na kurehemu tena;
Hushusha
hata kuzimu, na kuinua tena;
Wala
hakuna awezaye kujiepusha na mkono wake. (K)
Enyi
bani Israeli, mshukuruni mbele ya mataifa
Yeye
ambaye ametutawanya katikati yao. (K)
Kuko
huko utangazeni ukuu wake,
Mwadhimisheni
mbele ya wote walio hai;
Kwa
kuwa Yeye ndiye Bwana wetu,
Naye
Mungu yu Baba wetu,
Naye
Mungu yu Baba yetu milele. (K)
________
SHANGILIO
Aleluya,
aleluya,
Ee
Mungu, tunakusifu, tunakukiri kuwa Bwana. Jamii tukufu ya Mitume inakusifu.
Aleluya.
________
INJILI
Lk.
9:1-6
Yesu
aliwaita wale Thenashara, akawapa uwezo na mamlaka juu ya pepo wote na kuponya
maradhi. Akawatuma wautangaze ufalme wa Mungu, na kupoza wagonjwa. Akawaambia,
Msichukue kitu kwa safari yenu, fimbo, wala mkoba, wala mkate, wala fedha, wala
mmoja wenu asiwe na kanzu mbili. Na nyumba yoyote mtakayoingia kaeni humo,
tokeni humo. Na wale wasiowakaribisha, mtokakpo katika mji huo yakung’uteni
hata mavumbi ya miguuni mwenu, kuwa ushuhuda juu yao. Wakaenda, wakazunguka
katika vijiji, wakihubiri Injili, na kupoza watu kila mahali.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
-------------------------
Copyright © 2020,
"MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora –
Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment