MASOMO
YA MISA, SEPTEMBA 21, 2021
JUMANNE
YA 25 YA MWAKA
SIKUKUU
YA MT. MATHAYO, MTUME NA MWINJILI
SOMO
1
Efe.
4:1 – 7, 11 – 13
Nawasihi,
mimi niliye mfungwa katika Bwana, mwenende kama inavyoustahili wito wenu
mlioitiwa; kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika
upendo; na kujitahidi kuuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani, mwili
mmoja, na Roho mmoja, Imani moja, ubatizo mmoja. Mungu mmoja, naye ni Baba wa
wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote. Lakini kila mmoja wenu
alipewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa chake Kristo. Naye alitoa wengine
kuwa mitume; na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti; na wengine
kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi
ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; hata na sisi sote
tutakapoufikia umoja wa Imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu
mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
19:1 – 4 (K) 4
(K)
Sauti yao imeenea duniani mwote.
Mbingu
zauhubiri utukufu wa Mungu,
Na
anga laitangaza kazi ya mikono yake.
Mchana
husemezana na mchana,
Usiku
hutolea usiku maarifa. (K)
Hakuna
lugha wala maneno,
Sauti
yao haisikilikani.
Sauti
yao imeenea duniani mwote,
Na
maneno yao hata miisho ya ulimwengu. (K)
SHANGILIO
Aleluya,
aleluya,
Ee
Mungu, tunakusifu, tunakukiri kuwa Bwana. Jamii tukufu ya Mitume inakusifu.
Aleluya.
INJILI
Mt.
9:9 – 13
Yesu
alipokuwa akipita aliona mtu ameketi forodhani, aitwaye Mathayo, akamwambia,
Nifuate. Akaondoka, akamfuata. Ikawa alipoketi nyumbani ale chakula, tazama,
watoza ushuru wengi na wenye dhambi walikuja wakaketi pamoja na Yesu na
wanafunzi wake. Mafarisayo walipoona, waliwaambia wanafunzi wake, Mbona mwalimu
wenu anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi? Naye aliposikia,
aliwaambia, Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi. Lakini nendeni,
mkajifunze maana yake maneno haya, Nataka rehema, wala si sadaka; kwa maana
sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
-------------------------
Copyright © 2020,
"MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora –
Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment