MASOMO YA MISA, SEPTEMBA
17, 2021
IJUMAA, JUMA LA 24 LA
MWAKA
SOMO 1
1Tim. 6:2-12
Mambo hayo uyafundishe na
kuonya. Mtu awaye yote akifundisha elimu nyingine, wala hayakubali maneno yenye
uzima ya Bwana wetu Yesu Kristo, wala mafundisho yapatanayo na utauwa,
amejivuna; wala hafahamu neno lolote; bali ana wazimu wa kuwazia habari za
maswali, na mashindano ya maneno, ambayo katika hayo hutoka husuda, na ugomvi,
na matukano, na shuku mbaya; na majadiliano ya watu walioharibika akili zao,
walioikosa kweli, huku wakidhani ya kuwa utauwa ni njia ya kupata faida.
Walakini utauwa pamoja na kuridhika ni faida kubwa. Kwa maana hatukuja na kitu
duniani, tena hatuwezi kutoka na kitu; ila tukiwa na chakula na nguo
tutaridhika na vitu hivyo.
Lakini hao watakao kuwa
na mali huanguka katika majaribu na tanzi, na tamaa nyingi zisizo na maana,
zenye kudhuru, ziwatosazo wanadamu katika upotevu na uharibifu. Maana shina
moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani
hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi.
Bali wewe, mtu wa Mungu,
uyakimbie mambo hayo; ukafuate haki, utauwa, Imani, upendo, saburi, upole. Piga
vita vile vizuri vya Imani; shika uzima ule wa milele ulioitiwa, ukaungama
maungamo mazuri mbele ya mashahidi wengi.
Neno la Bwana… Tumshukuru
Mungu.
________
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 49:5-9, 16-19 (K)
Mt. 5:3
(K) Heri walio maskini
war oho, maana ufalme wa mbinguni ni wao.
Kwa nini niogope siku za
uovu,
Ubaya ukinizunguka
miguuni pangu?
Wa hao wanaozitumainia
mali zao,
Na kujisifia wingi wa
utajiri wao. (K)
Hakuna mtu awezaye
kumkomboa ndugu yake,
Wala kumpa Mungu fidia
kwa ajili yake,
Maana fidia ya nafsi zao
ina gharama,
Wala hana budi kuiacha
hata milele.
Ili ishi sikuzote
asilione kaburi. (K)
Usiogope mtu atakapopata
utajiri
Na fahari ya nyumba yake
itakapozidi.
Maana atakapokufa
hatachukua chochote;
Utukufu wake hautashuka
ukimfuata. (K)
Ajapojibariki nafsi yake
alipokuwa hai,
Na watu watakusifu
ukijitendea mema,
Atakwenda kwenye kizazi
cha baba zake,
Hawataona nuru hata
milele. (K)
________
SHANGILIO
Zab. 19:8
Aleluya, aleluya,
Amri ya Bwana ni safi,
huyatia macho nuru.
Aleluya.
________
INJILI
Lk. 8:1 – 3
Yesu alikuwa
akizunguka-zunguka katika miji na vijiji akihubiri na kuitangaza habari njema
ya ufalme wa Mungu; na wale Thenashara walikuwa pamoja naye, na wanawake kadha
wa kadha ambao walikuwa na pepo wabaya na magonjwa wakaponywa; nao ni Mariamu
aitwaye Magdalene aliyetokwa na pepo saba, na Yohana mkewe Kuza, wakili wake Herode,
na Susana, na wengine wengi, waliokuwa wakimhudumia kwa mali zao.
Neno la Bwana… Sifa kwako
Ee Kristo..................
Copyright © 2020,
"MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora –
Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see
www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment