ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku 17,
2021,
Juma la 24 la Mwaka
1 Tim 6: 2-12;
Zab 48: 6-10, 17-20;
Lk 8: 1-3
KUWA NA YESU!
Luka anatuambia kuhusu
kazi kubwa waliyo ifanya idadi kubwa ya wanawake katika kutegemeza utume wa
Bwana wetu na Wafuasi. Pamoja na tofauti zao kati ya wanawake, lakini
inaonekana wote walikuwa na kitu cha pamoja kwamba: Yesu amewaponya kimiujiza
kwasababu ambayo hakuna jibu sahihi kutoka kwa Mwanadamu. Katika hali ya
kufikirika, kundi lililo fuatana na Yesu lilitoa ushahidi na kumtambulisha Yesu
kama Kristo Masiha. Wanawake hawa hawakuwa watu wasiojitambua waliofuata tu,
walikuwa watu waliokuwa hai katika kutangaza Injili ya Ufalme wa Mungu. Wakati
Yesu alivyo watuma wale kumi na wawili (Lk 9: 1-6) na wale sabini na mbili (Lk
10: 1-12). Aliwaambia wasichukue chochote. Hii ni kwasababu walikuwa wafanye
utume kwa wale waliowafuata, ambao kati yao waliishi miongoni mwao. Tunapaswa
tuwe tunafanya walichofanya wanawake hawa. Walimpenda Yesu sana, walimtumikia
yeye na wafuasi wake kwa vile walivyokuwa navyo.
Je unadhani Yesu
alihitaji msaada wao? Hapana. je, alihitaji chakula chao? Hapana. Kama Yesu
angependa angeweza kuchukua tu kipande cha mkate katika mkoba, na pale watakapo
hisi njaa yeye na wafuasi wake Yesu angeiongeza hata kuwa kikapu kilicho jaa.
Kwanini hakufanya hivyo? Hii ni kwasababu kama kuna kitu anachopenda Yesu zaidi
kuliko kuwalisha watu, ni wakati watu wanampa yeye kwasababu wanampenda.
Haitaji yote hayo, bali anapenda kupokea. Inampa furaha kubwa tukimpenda. Yesu
hajapungukiwa chochote, tukimpenda na kumtumikia ni faida kwetu sisi kwamba
tunampendeza Bwana, nasi tunajipatia Baraka kwa ajili ya roho zetu. Tunajua
kwamba sala zetu hazi muongezei Mungu kitu, ila za faa kwa ajili ya wokovu
wetu. Tumtumikie Mungu kwa uchaji katika wema na kweli ili tujipatie utakatifu
wa roho zetu.
Sala: Bwana, ninaomba uje
unisamehe mimi, niponye mimi nikurudie wewe kwa shukrani kuu, nikufuate wewe
popote pale uniongozapo. Yesu nakuamini wewe. Amina
------------------------
Copyright ©2013-2020
©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment