MASOMO YA MISA, SEPTEMBA
14, 2021
JUMANNE, JUMA LA 24 LA
MWAKA
SIKUKUU YA KUTUKUKA KWA
MSALABA
SOMO 1
Hes. 21:4 – 9
Siku zile jangwani, watu
walimnung’unikia Mungu, na Musa, mbona mmetupandisha huku kutoka nchi ya Misri,
ili tufe jangwani? Maana hapana chakula, wala hapana maji, na roho zetu
zinakinai chakula hiki dhaifu. Bwana akatuma nyoka za moto kati ya watu,
wakawauma, watu wengi wakafa. Watu wakamwendea Musa, wakasema, tumefanya dambi
kwa sababu tumemnung’unukia Mungu, na wewe, utuombee kwa Bwana, atuondolee
nyoka hawa. Basi, Musa akawaombea watu. Bwana akawaambia Musa, Jifanyie nyoka
ya shaba, ukaiweke juu ya mti, na itakuwa kila mtu aliyeumwa, aitazamapo,
ataishi. Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti, hata ikiwa nyoka
amemwuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya shaba, akaishi.
Neno la Bwana… Tumshukuru
Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 78:1 – 2, 34 – 38
(K) 7
(K) Msiyasahau matendo ya
Mungu.
Enyi watu wangu,
sikilizeni sheria yangu,
Tegeni masikio kwa maneno
ya kinywa changu.
Na nifunue kinywa changu
kwa mithali,
Niyatamke mafumbo ya
kale. (K)
Alipowaua ndipo
walipokuwa wakimtafuta;
Wakarudi wakamtaka Mungu
kwa bidii.
Wakakumbuka kuwa Mungu ni
mwamba wao,
Na Mungu Aliye juu ni
mkombozi wako. (K)
Lakini walimdanganya kwa
vinywa vyao,
Wakamwambia uongo kwa
ndimi zao.
Kwa maana mioyo yao
haikuwa thabiti kwake,
Wala hawakuwa waaminifu
katika agano lake. (K)
Lakini Yeye, kwa kuwa
anayo rehema,
Husamehe uovu wala
haangamizi.
Mara nyingi huipishia
mbali ghadhabu yake,
Wala haiwashi hasira yake
yote. (K)
SOMO 2
Fil. 2:6 – 11
Yesu Kristo alikuwa yuna
namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha
kushikamana nacho; bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa,
akawa ana mfano wa wanadamu; tena, alipoonekana ana umbo kama wanadamu,
alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba. Kwa hiyo tena
Mung alimwadhimisha mno, akamkirimia jina lile lipitalo kila jina, ili kwa jina
la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini
ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa Yesu Kristo ni Bwana, kwa utukufu wa Mungu
Baba.
Neno la Bwana… Tumshukuru
Mungu.
SHANGILIO
Aleluya, aleluya,
Ee Kristu tunakuabudu na kukutukuza,
kwa kuwa umeikomboa dunia kwa msalaba wako.
Aleluya.
INJILI
Yn. 3:13 – 17
Yesu alimwambia Nikodemo:
Hakuna mtu aliyepaa mbinguni, ila yeye aliyeshuka kutoka mbinguni, yaani, Mwana
wa Adamu. Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana
wa Adamu hana budi kuinuliwa; ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele
katika yeye. Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa
Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa
milele. Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali
ulimwengu uokolewe katika yeye.
Neno la Bwana… Sifa kwako
Ee Kristo.
-------------------------
Copyright © 2020,
"MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora –
Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see
www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment