MASOMO YA MISA, JUMATATU 27, 2021.
JUMA
LA 26 LA MWAKA
SOMO
1.
Zekaria
8:1-8
Neno
la BWANA wa majeshi likanijia, kusema,
BWANA
wa majeshi asema hivi, Mimi nina wivu kwa ajili ya Sayuni, wivu mkuu, nami nina
wivu kwa ajili yake kwa ghadhabu kuu.
BWANA
asema hivi, Mimi nimerudi Sayuni, nami nitakaa katikati ya Yerusalemu; na
Yerusalemu utaitwa, Mji wa kweli; na Mlima wa BWANA wa majeshi utaitwa, Mlima
mtakatifu.
BWANA
wa majeshi asema hivi, Wazee wanaume na wazee wanawake watakaa tena katika njia
za Yerusalemu, kila mtu ana mkongojo wake mkononi, kwa kuwa ni mzee sana.
Na
hizo njia za mji zitajaa wavulana, na wasichana, wakicheza katika njia zake.
BWANA
wa majeshi asema hivi, Ingawa hili ni neno lililo gumu mbele ya macho ya mabaki
ya watu hawa katika siku hizo, je! Liwe neno gumu mbele ya macho yangu? Asema
BWANA wa majeshi.
BWANA
wa majeshi asema hivi, Tazama, nitawaokoa watu wangu toka nchi ya mashariki, na
toka nchi ya magharibi;
nami
nitawaleta, nao watakaa katikati ya Yerusalemu; nao watakuwa watu wangu, nami
nitakuwa Mungu wao, katika kweli na katika haki.
Neno
la Bwana...........Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI.
Zaburi
102:16-18.19-21.29 and 22-23 (R. 17)
(K)BWANA
atakapokuwa ameijenga Sayuni,
Atakapoonekana
katika utukufu wake,
Kisha
mataifa wataliogopa jina la BWANA,
Na
wafalme wote wa dunia utukufu wako;
BWANA
atakapokuwa ameijenga Sayuni,
Atakapoonekana
katika utukufu wake,
Atakapoyaelekea
maombi yake aliye mkiwa,
Asiyadharau
maombi yao.(K)
Kizazi
kitakachokuja kitaandikiwa hayo,
Na
watu watakaoumbwa watamsifu BWANA.
Maana
ametazama toka patakatifu pake pa juu,
Toka
mbinguni BWANA ameiangalia nchi,
Ili
akusikie kuugua kwake aliyefungwa,
Na
kuwafungua walioandikiwa kufa.(k)
Wana
wa watumishi wako watakaa,
Na
wazao wao wataimarishwa mbele zako.
Watu
walitangaze jina la BWANA katika Sayuni,
Na
sifa zake katika Yerusalemu,
Pindi
mataifa watapokusanyika pamoja,
Falme
nazo ili kumtumikia BWANA.(K)
SHANGILIO.
Marko
10:45
Alleluia
Alleluia!!
Kwa
maana Mwana wa Adamu naye hakuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake
iwe fidia ya wengi.
Alleluia!
INJILI
Luka
9:46-50
Wakaanza
kuhojiana, ni nani atakayekuwa mkubwa miongoni mwao.
Naye
Yesu alipotambua mawazo ya mioyo yao, alitwaa mtoto mdogo akamweka karibu naye,
akawaambia,
Ye yote atakayempokea mtoto huyu kwa jina langu anipokea mimi; na ye yote
atakayenipokea mimi ampokea yeye aliyenituma. Kwa kuwa aliye mdogo miongoni
mwenu nyote huyo ndiye mkubwa.
Yohana
akajibu akamwambia; Bwana mkubwa, tuliona mtu anatoa pepo kwa jina lako;
tukamkataza, kwa sababu hafuatani na sisi.
Yesu
akamwambia, Msimkataze, kwa kuwa yeye ambaye si kinyume chenu yu upande wenu.
Neno
la Bwana.........Sifa kwako ee kristo.
-------------------------
No comments:
Post a Comment