“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya Kila siku
Jumatatu,
Sptemba 27, 2021,
Juma
la 26 la Mwaka
Zek
8: 1-8;
Zab
102:16-18.19-21.29 and 22-23 (R. 17)
Lk
9: 46-50
Hakika
Mungu anao uwezo mkuu sana.
Karibuni
sana wapendwa wa Bwana kwa adhimisho la misa takatifu asubuhi ya leo. Neno la
Bwana katika somo la kwanza Nabii Zekaria anatoa unabii kwa taifa la Yuda
lililorudi utumwani. Lilikuta nchi yao na mji wao wa Yerusalem ukiwa katika
mahame na magofu. Wengi waliuawa na miili yao kutupwa hadharani. Mwenyezi Mungu
anaeleza kwamba hali itabadilika, watu watazaliwa tena wapya na kuishi muda
mrefu, miji itajengwa tena upya, matajiri watatokea tena, namna ambayo itazidi
ile ya mwanzoni.
Huu
ndio unabii anaoutoa Zekaria. Hakika Mwenyezi Mungu anao uwezo mkubwa; aweza
kufanya mengi bila hata ya sisi kumsaidia. Aweza kuanzisha wanadamu wengine
hata bila ya sisi. Hakika Mungu anao uwezo mkuu sana. Tujifunze kumrudia na
kumtukuza Mwenyezi Mungu. Kila siku wanadamu wanazaliwa upya, tena wenye uwezo
kuliko sisi. Wanaojidai kuwa na uwezo sasa watashangaa kuona kwamba watazaliwa
wengine wenye uwezo kutushinda sisi. Hivyo tukiwa na afya zetu, tukiwa na muda
wetu, na vipaji vyetu, tumtumikie Mungu. Tusijivune au kutumia kile tupewacho
na Mungu kumtesa jirani yetu.
Wanadamu
ni kama ua lichanualo, wakati huu tunaonekana kuwa wazuri, ipo siku tutazimika.
Tuwezacho kujivunia ni kwa jinsi gani tulivyoweza kuishi karibu zaidi na
Mwenyezi Mungu. Ni wema gani niliompa mtoto, jirani au rafiki yangu au aliye na
shida. Tujifunze kutumia muda wetu, na afya yetu vyema.
Pia
ujumbe huu utufae na sisi ambao tumewahi kupoteza mali, kuibiwa, au kufilisika.
Tutambue kwamba Mwenyezi Mungu aweza kutujaza tena mema yake, mambo yakawa tena
mazuri zaidi hata kuliko zamani. Tumwombe Mwenyezi Mungu apate kubadilisha hali
yetu na kuwa mpya zaidi.
Katika
somo la injili, Yesu anatueleza kwamba aliye mdogo miongoni mwetu sote, ndiye
aliye mkubwa. Mdogo ndiye anayetumikia, mara nyingi, wafalme hawatumikii bali
watumwa wao, walio na cheo cha chini na kipato cha chini. Yesu anadai hawa ndio
walio wakubwa mbele yake. Anayetumikia hupokea fadhila, na rehema machoni pa
Bwana. Kukubali kumtumikia mwenzako ni kuonesha uaminifu kwa mambo yaliyo
madogo na Mwenyezi Mungu humkabidhi yeyote anayeonesha uaminifu kwa mambo
madogo hukabidhiwa mambo makubwa.
Tunapoonesha
uaminifu kwa kuwatumikia wenzetu, Mwenyezi Mungu atatukabidhi yaliyo makubwa
zaidi. Sisi tusichoke kuonesha uaminifu kwa kuwahudumia wenzetu. Tumsifu Yesu
Kristo.
------------------------
Copyright ©2013-2020
©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment