MASOMO
YA MISA
JUMATANO,
SEPTEMBA 29, 2021
JUMA
LA 26 LA MWAKA
SIKUKUU
YA WATAKATIFU MIKAELI, GABRIELI NA RAFAELI, MALAIKA WAKUU
SOMO
I
Dan.
7:9-10,13-14
Nilitazama
viti vya enzi vikawekwa, na mmoja aliye mzee wa siku ameketi; mavazi yake
yalikuwa meupe kama theluji, na nywele za kichwa chake kama sufu safi; kiti chake
cha enzi kilikuwa miali ya moto, na gurudumu zake moto uwakao. Mto kama wa moto
ukatoka ukapita mbele zake, maelfu elfu wakamtumikia, na elfu kumi wakasimama
mbele zake; hukumu ikawekwa, na vitabu vikafunuliwa.
Nikaona
katika njozi za usiku, na tazama mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja pamoja na
mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku, wakamleta karibu naye. Naye
akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote,
na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele ambayo haitapita
kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa.
Neno
la Mungu… Tumshukuru Bwana.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
138:1-5 (K) 1
(K)
Mbele ya miungu nitakuimbia zaburi.
Nitakushukuru
kwa moyo wangu wote,
Mbele
ya miungu nitakuimbia zaburi.
Nitasujudu
nikilikabili hekalu lako takatifu. (K)
Kwa
ajili ya fadhili zako na uaminifu wako,
Kwa
maana umeikuza ahadi yako,
Kuliko
jina lako lote.
Siku
ile niliyokuita uliniitikia,
Ukanifariji
nafsi kwa kunitia nguvu. (K)
Ee
Bwana, wafalme wote wa dunia watakushukuru,
Watakapoyasikia
maneno ya kinywa chako.
Naam,
wataziimba njia za Bwana,
Kwa
maana utukufu wa Bwana ni mkuu (K)
SHANGILIO
Zab.
105:3
Aleluya,
aleluya,
Mhimidini
Bwana, enyi majeshi yake yote,
ninyi
watumishi wake mfanyao mapenzi yake.
Aleluya.
INJILI
Yn.
1:47-51
Yesu
alipomwona Nathanaeli anakuja kwake akanena habari zake, Tazama, Mwisraeli
kweli kweli, hamna hila ndani yake. Nathanaeli akamwambia, Umepataje
kunitambua? Yesu akajibu, akamwambia, Kabla Filipo hajakuita, ulipokuwa chini
ya mtini nilikuona. Nathanaeli akamjibu, Rabi, wewe u Mwana wa Mungu, ndiwe
Mfalme wa Israeli. Yesu akajibu, akamwambia, kwa sababu nilikuambia, Nilikuona
chini ya mtini, waamini? Utaona mambo makubwa kuliko haya. Akawaambia, Amin,
amin, nawaambia, Mtaziona mbingu zimefunguka na malaika wa Mungu wakikwea na
kushuka juu ya Mwana wa Adamu.
Neno
la Bwana...Sifa kwako, ee Kristo
-------------------------
Copyright © 2020,
"MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora –
Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment