“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Jumatano,
Septemba 29, 2021.
Juma
la 26 la Mwaka
Sikukuu
ya Watakatifu Malaika Wakuu, MIKAEL, GABRIELI NA RAFAELI
Dan
7: 9-10, 13-14 au Ufu 12: 7-12
Zab
137: 1-5
Yn
1: 47-51
JESHI
LA MBINGUNI!
MALAIKA
KATIKA MAISHA YETU!
Leo
tuna adhimisha sikukuu ya Malaika wakuu watatu ambao majina yao yanatajwa
katika maandiko: Mikaeli, Gabriel na Rafaeli. Hawa malaika wanaitwa “Malaika
Wakuu” maana yake ni wakuu kwasababu wana utume maalumu waliopewa na Mungu.
Sikukuu hii ya malaika inatukumbusha kwamba vitu vinavyo onekana na kushikika
ni sehemu ndogo sana ya ukweli halisi na hatuwezi kujifanya kujua kila kitu.
Siku hizi tunaweza tusitembelewe na malaika kama alivyomtembelea Bikira Maria
wakati wakutangazwa kuzaliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo au kipindi cha
kutangaza ufufuko wa Yesu, au kipindi cha Tobiti, lakini Mungu anaendelea
kuwasiliana nasi kwa namna ya pekee. Swali ni kwamba, mimi nipo wazi kiasi
ghani Mungu anapotaka kuongea nami? Hasa kwa njia ya neno lake? Je unaamini
uwepo wa malaika hawa, je unaomba wakuombee? Mungu anataka kuwatumia, tafuta
msaada wao katika maisha yako.
Leo
sala yetu iwe, Baba wa Mbinguni, umetupa malaika wakuu ili kutusaidia sisi
wahujaji hapa duniani. Mtakatifu Malaika Mikaeli ni kinga yetu, namuomba aje
kunisaidia, awapiganie wapendwa wangu wote, na atukinge na hatari. Mtakatifu
Malaika Gabrieli ni mjumbe wa habari njema, namuomba anisaidie kusikia sauti yako
na anifundishe ukweli. Mtakatifu Malaika Rafaeli ni malaika anaye ponya,
ninamuomba anipe uponyaji wa yale yote ninayohitaji kuponywa na ya kila mmoja
ninaye mfahamu, nyanyua juu katika kiti chako cha neema na utupe tena zawadi
yako ya kupona na kuwa huru. Tusaidie Bwana tuweze kutambua kwa ukamilifu
kabisa, ukweli wa Malaika Wakuu na hamu yao yakutaka kututumikia.
Sala:
Baba wa Mbinguni, umetupa malaika wakuu ili kutusaidia sisi wahujaji hapa
duniani. Mtakatifu Malaika Mikaeli ni kinga yetu, namuomba aje kunisaidia,
awapiganie wapendwa wangu wote, na atukinge na hatari. Mtakatifu Malaika
Gabrieli ni mjumbe wa habari njema, namuomba anisaidie kusikia sauti yako na
anifundishe ukweli. Mtakatifu Malaika Rafaeli ni malaika anaye ponya,
ninamuomba anipe uponyaji wa yale yote ninayohitaji kuponywa na ya kila mmoja
ninaye mfahamu, nyanyua juu katika kiti chako cha neema na utupe tena zawadi
yako ya kupona na kuwa huru. Tusaidie Bwana tuweze kutambua kwa ukamilifu
kabisa, ukweli wa Malaika Wakuu na hamu yao yakutaka kututumikia. Malaika
Watakatifu, Mtuombee. Amina.
------------------------
Copyright ©2013-2020
©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment