MASOMO YA MISA,
JUMATANO, SEPTEMBA 15,
2021
JUMA LA 24 LA MWAKA
KUMBUKUMBU YA BIKIRA
MARIA MTAKATIFU WA MATESO
SOMO 1
Ebr. 5:7 – 9
Kristo, siku hizo za
mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na
dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa wa jinsi alivyokuwa mcha
Mungu; na, ingawa ni Mwana, alijifunza kutii kwa mates ohayo yaliyompata; naye
alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote
wanaomtii.
Neno la Bwana… Tumshukuru
Mungu.
________
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 31:1 – 5, 14 – 15,
19 (K) 16
(K) Uniokoe, Ee Bwana,
kwa ajili ya fadhili yako.
Nimekukimbilia Wewe,
Bwana,
Nisiaibike mbele kwa haki
yako uniponye.
Unitegee sikio lako,
uniokoe hima. (K)
Uwe kwangu mwamba wa
nguvu,
Nyumba yenye maboma ya
kuniokoa,
Ndiwe genge langu na
ngome yangu,
Kwa ajili ya jina lako
uniongoze, unichunge. (K)
Utanitoa katika wavu
walionitegea kwa siri,
Maana wewe ndiwe ngome
yangu.
Mikononi mwako naiweka
roho yangu,
Umenikomboa, Ee Bwana,
Mungu wa kweli. (K)
Lakini mimi nakutumaini
Wewe, Bwana,
Nimesema, Wewe ndiwe
Mungu wangu.
Nyakati zangu zimo
mikononi mwako;
Uniponye na adui zangu,
nao wanaonifuatia. (K)
Jinsi zilivyo nyingi
fadhili zako
Ulizowawekea wakuchao;
Ulizowatendea
wakukimbiliao
Mbele ya wanadamu! (K)
________
SHANGILIO
Aleluya, aleluya,
Bikira Maria anafurahi
yeye ameshinda na kupata nishani ya ushahidi pasipo kufa, alipokuwa chini ya
msalaba wa Bwana.
Aleluya.
________
INJILI
Yn. 19:25 – 27
Penye msalaba wake Yesu
walikuwa wamesimama mamaye, na umbu la mamaye, Mariamu wa Klopa, na Mariamu
Magdalene. Basi Yesu alipomwona mama yake, na yule mwanafunzi aliyempenda
amesimama karibu, alimwambia mama yake, Mama, tazama, mwanao. Kisha akamwambia
yule mwanafunzi, Tazama, mama yako. Na tangu saa ile mwanafunzi yule akamchukua
nyumbani mwake.
Neno la Bwana… Sifa kwako
Ee Kristo.
Au
INJILI
Lk. 2:33 – 35
Babaye na mamaye wa Yesu
walikuwa wakiyastaajabia hayo yaliyonenwa juu yake. Simeoni akawabariki,
akamwambia Mariamu mama yake, Tazama, huyu amewekwa kwa kuanguka na kuinuka
wengi walio katika Israeli, na kuwa ishara itakayonenewa. Nawe mwenyewe, upanga
ukaingia moyoni mwako, ili yafunuliwe mawazo ya mioyo mingi.
Neno la Bwana… Sifa kwako
Ee Kristo.
-------------------------
Copyright © 2020,
"MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora –
Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see
www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment