“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Ijumaa, Septemba 15,
2021,
Juma la 24 la Mwaka wa
Kanisa
Kumbukumbu ya Bikira
Maria Mtakatifu wa Mateso
Ebr 5: 7-9; au 1Kor
15:1-11
Zab 30: 2-6, 15-16, 20;
Yn 19: 25-27, 35 au Lk 2:
33-35
KUTESEKA KWA AMANI NA
FURAHA!
Leo tunakumbuka mateso ya
Mama yetu Bikira Maria. Mateso ya Maria yalikuwa ya ndani. Bikira Maria alikuwa
mwanadamu kamili kwasababu hakutenda dhambi na kati ya watu waliompendeza Mungu
katika hali ya ukamilifu wote ni Bikira Maria licha ya Mwanae, lakini kwa ajili
ya hili hatuwezi kusema hakuwa na hisia ya kuhisi mambo ya duniani. Kwasababu
ya ukamilifu wake, alipenda kwa mapendo ya ndani kuliko sisi. Kwasababu ya
upendo huu, alihisi uchungu wa kumpoteza mwanae kuliko sisi. Mateso ya Maria
tofauti na yetu yalikuwa kamili. Mateso yetu mara nyingi yamechanganyika na
udhaifu wetu. Maria hakuhuzunika kwasababu atamkosa Mwanae ampe msaada.
Aliteseka kwasababu aliona mateso ya yule anaye mpenda, na akahisi mateso yale
kama Mwanae alivyohisi. Tunaweza kuhisi pia ni kwa jinsi ghani Yesu
alivyojisikia alivyomuona Mamaye katika huzuni. Ni hakika ilimsababishia mateso
pia, lakini ilikuwa pia ni hali ya kuonesha ukaribu wao. Ulimwengu mzima
unaweza kuwa umekuwa wa ukatili na hali zote, lakini uso wa Mama yake ulikuwa
ni sehemu pekee alioweza kuelekezea macho yake, akiona sura na mfano aliouweka
wakati anatuumba sisi.
Huzuni ya mama haikuwa ni
huzuni bila matumaini. Alijua kwa matumani fulani kwamba Mwanae atafufuka
kutoka wafu. Tumaini lake halikumzuia kuhisi uchungu na wala halikumzuia
kutazamia ufufuko wake. Maria ni Mama yetu. Kama ilivyo kwa Mama mwema,
anatufundisha sisi. Tunapaswa tutuoe muda wetu tukiwa naye katika mti wa
Msalaba, tukimuomba atufundishe jinsi ya kuhisi nasi mateso yetu katika maisha.
Tusisite kumkimbilia atuombee tunapokumbana na adha na mateso katika maisha,
yeye awe faraja na msaada wetu kwani atakuwa nasi, akisimama nasi na kuteseka
nasi, akiyaweka yote chini ya Msalaba wa Mwanae kwa niaba yetu.
Sala: Mama wa Upendo,
Mama wa Mateso na Mama wa huruma, utuombee sisi. Amina
------------------------
Copyright ©2013-2020
©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment