MASOMO YA MISA,
JUMAMOSI, SEPTEMBA 18,
2021
JUMA LA 24 LA MWAKA
________
SOMO 1
1Tim. 6:13-16
Nakuagiza mbele za Mungu
anayevihifadhi hai vitu vyote, na mbele za Kristo Yesu, aliyeyaungama maungamo
mazuri yale mbele ya Pontio Pilato, kwamba uilinde amri hii pasipo mawaa,
pasipo lawama, hata kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo; ambako yeye kwa
majira yake atakudhihirisha, yeye aliyehimidiwa, Mwenye uweza peke yake, Mfalme
wa wafalme, Bwana wa mabwana; ambaye yeye peke yake hapatikani na mauti, amekaa
katika nuru isiyoweza kuharibiwa; wala hakuna mwanadamu aliyemwona, wala
awezaye kumwona. Heshima na uweza una yeye hata milele. Amina.
Neno la
Bwana...Tumshukuru Mungu
________
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 100 (K) 2
(K) Njoni mbele za Bwana
kwa kuimba.
Mfanyieni Bwana shangwe,
dunia yote;
Mtumikieni Bwana kwa
furaha;
Njoni mbele zake kwa
kuimba.(K.)
Jueni kwamba Bwana ndiye
Mungu;
Ndiye aliyetuumba na sisi
tu watu wake;
Tu watu wake, na kondoo
wa malisho yake. (K.)
Ingieni malangoni mwake
kwa kushukuru;
Nyuani mwake kwa kusifu;
Mshukuruni, lihimidini
jina lake.(K.)
Kwa kuwa Bwana ndiye
mwema;
Rehema zake ni za milele;
Na uaminifu wake vizazi
na vizazi.(K.)
________
SHANGILIO
Kol. 3:16,17
Aleluya, aleluya,
Neno la Kristo likae kwa
wingi
ndani yenu katika hekima
yote;
mkimshukuru Mungu Baba
kwa Yeye.
Aleluya.
________
INJILI
Lk. 8:4-15
Mkutano mkuu
ulipokutanika, na wale waliotoka kila mji wakimjia, Yesu alisema kwa mfano:
Mpanzi alitoka kwenda kupanda mbegu zake; naye alipokuwa akizipanda, nyingine
zilianguka karibu na njia, zikakanyagwa, ndege wa angani wakazila. Nyingine
zikaanguka penye mwamba; zilipoanza kumea zikakauka kwa kukosa rutuba. Nyingine
zikaanguka kati ya miiba, na miiba ikamea pamoja nazo ikazisonga. Nyingine
zikaanguka penye udongo mzuri; zikamea, zikazaa moja kwa mia. Alipokuwa akinena
hayo alipaza sauti akisema, Mwenye masikio ya kusikilia, na asikie. Wanafunzi
wake wakamwuliza, Maana yake nini mfano huo? Akasema, Ninyi mmepewa kuzijua
siri za ufalme wa Mungu; bali wengine kwa mifano, ili wakiona wasione, na
wakisikia wasielewe. Na huo mfano, maana yake ni hii; Mbegu ni neno la Mungu.
Wale wa karibu na njia ndio wasikiaopo hulipokea lile neno kwa furaha; nao
hawana mizizi, huamini kitambo kidogo, na wakati wa kujaribiwa hujitenga. Na
zilipoanguka penye miiba ni wale waliosikia, na katika kuenenda kwao husongwa
na shughuli na mali, na anasa za maisha haya, wasiivishe lolote. Na zile penye
udongo mzuri, ndio wale ambao kwa unyofu na wema wa mioyo yao hulisikia neno,
na kulishika; kisha huzaa matunda kwa kuvumilia.
Neno la Bwana...Sifa
kwako, ee Kristo
-------------------------
Copyright © 2020,
"MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora –
Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see
www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment