“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Jumamosi, Septemba 18,
2021
Juma la 24 la Mwaka
1 Tim 6: 13-16;
Zab 99: 1-5;
Lk 8: 4-15
KUMSIKILIZA MUNGU!
Somo la Injili
linatueleza leo kuhusu mfano wa mpanzi na kufuatwa na maana yake. Mbegu
inaoneshwa kama Neno la Mungu, wale walio pembezoni mwa barabara ni wale
wanaosikia na yule muovu huja na kulichukua neno kutoka ndani ya mioyo yao, ili
wasiweze kuamini.
Mfano huu hunyambulisha
njia nne ambazo tunasikia neno la Mungu . Wengine wapo kama njia, wengine kama
mwamba, wengine kama udongo uliosongwa na miiba, na wengine kama udongo mzuri. Kama
mfano wa haya yote kuna uwezekano wa kukuwa kwa neno la Mungu. Udongo mzuri ni
pale ambapo neno la Mungu linapokelewa na kuzaa matunda. Mbegu iliyosongwa na
miiba ni pale ambapo neno la Mungu linakuwa lakini matunda yanaondolewa na
matatizo ya kila siku na vishawishi. Hizi mbegu zilizo anguka kwenye mwamba
hukuwa lakini pale maisha yanapo kuwa magumu hukauka na kuacha kutoa matunda.
Mbegu za kwanza kuanguka njiani, ni za mwisho kabisa kutamanika kati ya zote.
Katika hali hii hata mbegu zenyewe hazikui. Ardhi inafanywa ngumu kiasi kwamba
hata haziwezi kuzama ndani. Hata njia yenyewe haiwezi kuleta mazingira mazuri
kuiruhusu kuota, na kama Injili inavyosema, yule muovu huja nakuiiba ile mbegu
hata kabla haijakuwa.
Tafakari njia mbali mbali
ambapo shetani anaweza kuja na kuliiba lile neno la Mungu ndani yako. Inaweza
kuwa katika hali ya kukuweka wewe na mambo mengi sana kiasi ambacho hupati muda
kabisa wa kuzamisha neno la Mungu ndani mwako. Au inaweza kuwa ni katika hali
ya kuruhusu kelele za ulimwengu zikusumbue na kulisonga lile neno na kushindwa
kuliacha lizame ndani. Bila kujali upo katika hali ghani, kilicho cha muhimu ni
kutengeneza mazingira mazuri ya kulisikiliza neno la Mungu na kulielewa. Hatua
hiyo ya kwanza inapo fanikiwa unaweza sasa ukaondoa, miamba na miiba kutoka
katika udongo wa roho yako.
Sala: Bwana, nisaidie
niweze kusikiliza neno lako, nilisikilize, kulielewaa na kuliamini. Nisaidie
moyo wangu uweze kuwa udongo mzuri ili liweze kuingia na kuzaa matunda mema.
Yesu nakuamini wewe. Amina
------------------------
Copyright ©2013-2020
©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment