“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Alhamisi, Agosti 19, 2021,
Juma la 20 la Mwaka
Amu 11: 29-39;
Zab 39: 5-10;
Mt 22:1-14
SHEREHE YA HARUSI!
Inafarijisha sana,
kufikiri mbinguni kama sehemu ya sherehe ya harusi/karamuni. Itakuwa Yesu aliipenda
sherehe ya harusi na akaona ni kielelezo/mfano mzuri wa kutueleza sisi alicho
tuandalia Mungu.
Katika somo la injili,
mfalme anashangazwa kwamba ameandaa sherehe kubwa ya harusi ya mtoto wake
lakini wageni walioalikwa hawana muda wakuhudhuria karamu hiyo. Kuna mambo
mengi katika mfano huu. Kwa hakika cha kwanza ni kuhusu kualikwa. Mungu
anatualika na hatulazimishi anatupa uhuru. Tunaweza kukubali au kukataa. Tupo
huru. Inavyoonekana alivyotendewa yule asiyevaa vazi la harusi inaweza
kushangaza kidogo. Tuliangalie hili kwa ukaribu zaidi. Wakati mfalme
anavyomtambua “alikaa kimya!” iko wazi kutoka kwenye somo kwamba huyu mtu
hakuwa na vazi la harusi kitendo cha kukosa kuwa makini na heshima kwa mfalme.
Si kwamba huyu mgeni alishindwa kuwa na vazi
Sisi tumealikwa kwenye
urafiki na Mungu. Tumepewa neema ya utakaso kama zawadi, lakini ni zawadi
inayohitaji kujishughulisha. Tunapaswa tuishi ujumbe wa Ukristo unaoweza
kutulazimu kubadili mitizamo yetu, tabia na aina ya maisha. Huyu mtu
aliyeelezwa kwenye injili hakuwa na lakusema. Hakuwa amejiandaa kuingia katika
karamu.
Mfano wa karamu
unaoendana sambamba na mfano huu ni Ekaristi Takatifu- zawadi ambayo ni ya hali
ya juu kabisa ambayo hatuwezi kujitetea kuwa haki yetu, zawadi tusio stahili.
Je, tunamaanisha kweli maneno tunayo sema kabla ya komunyo; Ee Bwana sistahili
uingie kwangu lakini sema neno tu na roho yangu itapona? Kwahiyo leo, tunaomba
mfano huu, ututikise mioyo yetu nakututoa katika uvivu na hali ya kuridhika na
hali yetu. Tusimchukulie Mungu kwa mizaha! Tumpende Mungu kweli tuwe tayari
kutoa sadaka yote yanayotufanya tujifariji binafsi na kushindwa kujiweka tayari
kwa karamu na hapo kiaminifu tuweze kusema kwa ujasiri “Kufanya mapenzi yako,
Ee Mungu, ndio furaha yangu”.
Sala: Ee Mungu, ninakushukuru
kwa kunialika kwenye karamu yako ya Mbinguni. Amina.
------------------------
Copyright ©2013-2020
©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment