MASOMO YA MISA,
JUMATANO, AGOSTI 18, 2021
JUMA LA 20 LA MWAKA
________
SOMO I
Amu 9: 6-15
Watu wote wa Shekemu
walikusanyika pamoja, na jamaa yote ya Milo, wakaenda na kumtawaza Abimeleki
awe mfalme, karibu na huo mgandi ulio karibu na ngome iliyo katika Shekemu.
Kisha walipomwambia huyo
Yothamu, yeye akaenda, akasimama juu ya kilele cha kilima cha Gerizimu, akapaza
sauti yake, akapiga kelele, na kuwaambia:
Nisikieni mimi, enyi watu
wa Shekemu, ili kwamba Mungu naye apate kuwasikia ninyi.
Siku moja miti ilitoka
ili kuutia mmoja mafuta uwe mfalme juu yao; ikauambia mti mzeituni, Tawala wewe
juu yetu.
Lakini huo mzeituni
ukaiambia, Je! Niache mafuta yangu, ambayo kwangu mimi watu wamheshimu Mungu na
wanadamu, ili niende nikayongeyonge juu ya miti?
Kisha miti ikauambia
mtini, Njoo wewe, utawale juu yetu.
Lakini huo mtini
ukaiambia, Je! Niuache utamu wangu, na matunda yangu mazuri, niende
nitayonge-yonge juu ya miti?
Kisha miti ikauambia
mzabibu, Njoo wewe, utawale juu yetu.
Huo mzabibu nao
ukaiambia, Je! Niiache divai yangu, ambayo humfurahisha Mungu na wanadamu, ili
niende nikayonge-yonge juu ya miti?
Ndipo hiyo miti yote
ikauambia mti wa miiba, Njoo wewe, utawale juu yetu.
Huo mti wa miiba
ukaiambia miti, Kwamba ninyi mwanitia mafuta niwe mfalme juu yenu kwelikweli,
basi njoni mtumaini kivuli changu; na kwamba sivyo, na utoke moto katika mti wa
miiba na kuitekete mierezi ya Lebanoni.
Neno la
Bwana...Tumshukuru Mungu
________
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 21: 1-6
(K) Ee Bwana, mfalme
atazifurahia nguvu zako.
Ee Bwana, mfalme
atazifurahia nguvu zako,
Na wokovu wako ataufanyia
shangwe nyingi sana.
Umempa haja ya moyo wake,
Wala hukumzuilia matakwa
ya midomo yake. (K)
Maana umesogezea Baraka
za heri,
Umemvika taji ya dhahabu
safi kichwani pake.
Alikuomba uhai, ukampa.
Muda mrefu wa siku
nyingi, milele na milele. (K)
Utukufu umemsogezea
Baraka za heri,
Umemvika taji ya dhahabu
safi kichwani pake.
Alikuomba uhai, ukampa.
Muda mrefu wa siku
nyingi, milele na milele. (K)
________
SHANGILIO
Zab 119:18
Aleluya, aleluya,
Unifumbue macho yangu
niyatazame
maajabu yatokayo katika
sheria yako.
Aleluya.
________
INJILI
Mt. 20: 1-16
Yesu aliwaambia wafuasi
wake: Ufalme wa mbinguni umefanana na mtu mwenye nyumba, aliyetoka alfajiri
kwenda kuajiri wakulima awapeleke katika shamba lake la mizabibu. Naye
alipokwisha kupatana na wakulima kuwapa kutwa dinari, aliwapeleka katika shamba
lake la mizabibu. Akatoka mnamo saa tatu, akaona wengine wamesimama sokoni
wasiokuwa na kazi; na hao nao akawaambia, Enendeni nanyi katika shamba langu la
mizabibu, na iliyo haki nitawapa. Wakaenda.
Akatoka tena mnamo saa
sita na saa kenda, akafanya vile vile. Hata kama saa kumi na moja akatoka,
akauta wengine wamesimama, akawaambia, Mbona mmesimama hapa mchana kutwa bila
kazi? Wakamwambia, Kwa sababu hakuna mtu aliyetuajiri. Akawaambia enendeni
nanyi katika shamba la mizabibu.
Kulipokuchwa, yule bwana
wa shamba akamwambia masimamizi wake, Waite wakulima, uwalipe ujira wao,
ukianzia wa mwisho hata wa kwanza. Na walipokuja wale wa saa kumi na moja,
walipokea kila mtu dinari. Na wale wa kwanza walipokuja, walidhani kwamba
watapokea zaidi; na hao pia wakapokea kila mtu dinari.
Basi wakiisha kuipokea,
wakamnung’unukia mwenye nyuma, wakisema, Hao wa mwisho wametenda kazi saa moja
tu, nawe umewasawazisha na sisi tuliostahimili taabu na hari za mchana kutwa.
Naye akamjibu mmoja wao, akamwambia, Rafiki, sikudhulumu; hukupatana nami kwa
dinari? Chukua iliyo yako, uende zako; napenda kumpa huyu wa mwisho sawa na
wewe. Si halali yangu kutumia vilivyo vyangu kama nipendavyo? Au jicho lako
limekuwa ovu kwa sababu ya mimi kuwa mwema Vivyo hivyo wa mwisho watakuwa wa
kwanza, na wa kwanza watakuwa wa mwisho.
Neno
la Bwana...Sifa kwako, ee Kristo
Copyright © 2020,
"MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora –
Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment