MASOMO YA MISA,
JUMAPILI, AGOSTI 15, 2021
JUMA LA 19 LA MWAKA
SHEREHE YA KUPALIZWA
MBINGUNI BIKIRA MARIA
SOMO 1
Ufu 11: 19, 12: 1-6, 10
Hekalu la Mungu lililoko
mbinguni likafunguliwa, na sanduku la agano lake likaonekana ndani ya hekalu
lake. Kukawa na umeme, na sauti, na radi, na tetemeko la nchi, na mnua ya mawe
nyingi sana.
Na ishara kuu ilionekana
mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu
ya kichwa chake taji ya nyota kumi na mbili. Naye alikuwa ana mimba, akilia,
hali ana utungu na kuumwa katika kuzaa.
Ikaonekana ishara
nyingine mbinguni; na tazama, joka kubwa jekundu, alikuwa na vichwa saba na
pembe kumi, na juu ya vichwa vyake vilemba saba. Na mkia wake wakokota theluthi
ya nyota za muinguni, na kuziangusha katika nchi. Na yule joka akasimama mbele
ya yule mwanamke aliye tayari kuzaa, ili azaapo, amle mtoto wake. Naye akazaa
mtoto mwanamume, yeye atakayewachunga mataifa yote kwa fimbo ya chuma. Na mtoto
wake akanyakuliwa hata kwa Mungu, na kwa kiti chake cha enzi. Yule mwanamke
akakimbilia nyikani, ambapo ana mahali palipotengenezwa na Mungu, ili wamlishe
huko muda wa siku elfu na mia mbili na sitini.
Nikasikia sauti kuu
mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na
mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye
awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.
Neno la Mungu...Tumshukuru
Mungu
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 45: 9-11, 15 (K) 10
(K) Mkono wako wa kuume
amesimama malkia. amevaa dhahabu ya Ofiri.
Binti za wafalme wamo
Miongoni mwa akina bibi
wako wastahiki.
Mkono wako wa kuume
amesimama malkia,
Amevaa dhahabu ya Ofiri.
Sikia, binti, utazame,
utege sikio lako,
Uwasahau watu wako na
nyumba ya baba yako. (K)
Naye mfalme atautamani
uzuri wako,
Maana ndiye bwana wako,
nawe umsujudie.
Watapelekwa kwa furaha na
shangwe,
Na kuingia katika nvumba
va mfalme. (K)
SOMO 2
1Kor 15: 20-26
Kristo amefufuka katika
wafu, limbuko lao waliolala. Maana kwa kuwa mauti ililetwa na mtu, kadhalika na
kiyama ya wafu ililetwa na mtu. Kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa,
kadhalika na katika Kristo wote watanuishwa. Lakini kila mmoja mahali pake;
limbuko ni Kristo; baadaye walio wake Kristo, atakapokuja. Hapo ndipo mwisho,
atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka
yote, na nguvu. Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke maadui wake wote chini
ya miguu yake. Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti.
Neno la
Mungu...Tumshukuru Mungu
SHANGILIO
Aleluya, aleluya,
Maria amepalizwa mbinguni
majeshi
yote ya malaika
wanafurahi.
Aleluya.
INJILI
Lk 1: 39-56
Mariamu aliondoka,
akaenda hata nchi ya milimani kwa haraka mpaka mji mmoja wa Yuda, akaingia
nyumbani kwa Zakaria akamwamkia Elisabeth Ikawa Elisabeti aliposikia kule
kuamkia kwake Mariamu, kitoto kichanga kikaruka ndani ya tumbo lake; Elisabeti
akajazwa Roho Mtakatifu; akapaza sauti kwa nguvu akasema, Umebarikiwa wewe
katika wanawake, naye mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Limenitokeaje neno hili,
hata mama wa Bwana wangu anijilie mimi? Maana sauti ya kuamkia kwako ilipoingia
masikioni mwangu, kitoto kichanga kikaruka kwa shangwe ndani ya tumbo langu.
Naye heri aliyesadiki; kwa maana yatatimizwa aliyoambiwa na Bwana.
Mariamu akasema,
Moyo wangu wamwadhimisha
Bwana,
Na roho yangu imemfurahia
Mungu,
Mwokozi wangu;
Kwa kuwa ameutazama
Unyonge wa mjakazi wake.
Kwa maana, tazama, tokea
sasa
Vizazi vyote wataniita mbarikiwa;
Kwa kuwa Mwenye nguvu
amenitendea makuu,
Na jina lake ni takatifu.
Na rehema zake hudumu
vizazi hata vizazi
Kwa hao wanaomcha.
Amefanya nguvu kwa mkono
wake;
Amewatawanya walio na
kiburi katika mawazo ya mioyo yao;
Amewaangusha wakuu katika
viti vyao vya enzi;
Na wanyonge amewakweza.
Wenye njaa amewashibisha
mema
Na wenye mali amewaondoa
mikono mitupu.
Amemsaidia Israeli,
mtumishi wake;
Ili kukumbuka rehema
zake;
Kama alivyowaambia baba
zetu,
Ibrahimu na uzao wake
hata milele.
Mariamu akakaa naye
kadiri ya miezi mitatu, kisha akarudi kwenda nyumbani kwake.
Neno la Bwana...Sifa
kwako, ee Kristo
Copyright © 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com
No comments:
Post a Comment