ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya kila siku
Jumatatu,
26 Julai, 2021,
Juma la 17 la Mwaka
Kut
32:15-24,30-34
Zab
106:19-23 (k) 1
Mt
13:31-35
UKUBWA
MACHONI MWA MUNGU
Karibuni
sana ndugu zangu kwa adhimisho la misa takatifu asubuhi ya leo. Leo tunaadhimisha
kumbukumbu ya Mt. Marta. Mtakatifu huyu anafahamika sana katika Biblia kwa
upendo wake kwa Yesu. Ndiye aliyemkaribisha Yesu nyumbani mwake akiwa na Maria
dada yake. Alionesha ukarimu wa hali ya juu kwa Yesu.
Alitaka
kumtumikia kwa nguvu zake zote kwa kumpatia mahitaji yake ya kimwili. Kosa la
Martha ni kwamba alitumia karibu muda wake wote kufanya haya, na mwishowe
alishindwa kupokea ujumbe Yesu aliomletea kwa kuja kwake. Alipomuona tu Yesu,
alihangaikia kutumikia bila hata kuuliza au kufuatilia kilichomleta. Hakika
Yesu hakuja kwa akina Maria na Martha hivihivi-alikuwa na ujumbe maalumu kwao
lakini Martha hakuhangaika kusikiliza ujumbe huu bali alikimbilia kukazania
kutumikia. Yesu anamwambia kwamba kwa kufanya hivi, anapoteza sehemu kubwa ya
kupata ujumbe toka kwake. Angalipaswa amsikilize Yesu kwanza. Yawezekana vile
alivyokuwa anaandaa, Yesu hakuvihitaji.
Kilichomtokea
Martha kinatutokea na sisi pia. Mara nyingi tunatumia muda wetu karibu wote
katika kuwahudumia wazazi wetu, watoto na wanafamilia wetu. Lakini hatupaswi
kutumia muda wetu wote katika kufanya kazi hizi tuu. Pawepo pia muda wa kukaa
karibu na Yesu, ili atufundishe namna ya kutumikia.
Tunaweza
kutumia nguvu zetu kutumikia lakini ikatokea kwamba kile tunachotumikia hakifai
chochote, au tunatumikia kwa namna isiyofaa, au tunatumikia lakini hakuna faida
ipatikanayo kwa sisi kutumika. Sisi tujitahidi kwenda mbele ya Yesu atufundishe
namna ya kutumikia ili basi huduma zetu zileta manufaa na matunda zaidi kwa
wale wanaotumikiwa.
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment