MASOMO
YA MISA, JULAI 26, 2021
JUMATATU,
JUMA LA 17 LA MWAKA
SOMO
1
Kut.
32:15-24, 30-34
Musa
aligeuka akashuka katika mlima, na zile mbao mbili za mawe mikononi mwake; mbao
ziliandikwa pande zote mbili, upande huu na upande huu ziliandikwa. Na zile mbao
zilikuwa kazi ya Mungu, nayo maandiko yalikuwa maandiko ya Mungu, yaliyochorwa
katika zile mbao.
Na
Yoshua aliposikia kelele za watu walipokuwa wakipiga kelele, akamwambia Musa,
Kuna kelele ya vita maragoni. Akasema, Hiyo si sauti ya watu wapigao kelele kwa
sababu ya kushinda vitani, wala si sauti ya watu wapigao kelele kwa sababu ya
kushindwa; bali kelele za watu waimbao nizo ninazozisikia mimi.
Hata
alipyakaribia marago akaiona ile ndama, na ile michezo. Hasira ya Musa ikawaka,
akazitupa zile mbao mikononi mwake, akazivunja chini ya mlima. Akaitwaa ile
ndama walioifanya, akaichoma moto, akaisaga hata ikawa mavumbi, akainyunyiza
juu ya maji, akawanywesha wana wa Israeli. Musa akamwambia Haruni; Watu hawa
wamekufanyani hata ukaleta dhambi hii kuu juu yao? Haruni akasema, Hasira ya
bwana wangu isiwake; wewe unawajua watu hawa, ya kuwa wamejielekeza kwa mabaya.
Maana waliniambia, Katufanyie miungu itakayokwenda mbele yetu, kwa maana mtu
huyo Musa, aliyetutoa katika nchi ya Misri, hatujui yaliyompata. Nikawaambia,
Mtu yeyote aliye na dhahabu na aivunje; basi wakanipa, nami nikaitupa ndani ya
moto, akatoka ndama huyu.
Basi
asubuhi yake Musa akawaambia watu, Mmetenda dhambi kuu; na sasa nitakwenda juu
kwa Bwana, labda nitafanya upatanisho kwa ajili ya dhambi yenu. Musa akarejea
kwa Bwana akasema, Aa! Watu hawa wametenda dhambi kuu, wamejifanyia miungu ya
dhahabu. Walakini sasa ikiwa utawasamehe dhambi yao – na kama sivyo, unifute,
nakusihi, katika kitabu chako ulichokiandika. Bwana akamwambia Musa, Mtu yoyote
aliyenitenda dhambi, ndiye nitakayemfuta katika kitabu changu. Basi sasa uende
ukawaongoze watu hawa mpaka mahali pale ambapo nimekuambia habari zake; tazama,
malaika wangu atakutangulia; pamoja na hayo siku nitakayowajilia nitawapatiliza
kwa ajili ya dhambi yao.
Neno
la Bwana... Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
106:19-23 (K) 1
(K)
Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema.
Walifanya
ndama huko Horebu,
Wakaisujudia
sanamu ya kuyeyuka.
Wakaubadili
utukufu wao,
Kuwa
mfano wa ng’ombe mla majani. (K)
Wakamsahau
Mungu, mwokozi wao,
Aliyetenda
makuu katika Misri.
Matendo
ya ajabu katika nchi ya Hamu,
Mambo
ya kutisha penye bahari ya Shamu. (K)
Akasema
ya kuwa atawaangamiza,
Kama
Musa, mteule wake, asingalisimama,
Mbele
zake kama mahali palipobomoka,
Ili
aigeuze hasira yake asije akawaharibu. (K)
SHANGILIO
Efe.
1:17, 18
Aleluya,
aleluya,
Mungu
wa Bwana wetu Yesu Kristu, awape roho ya hekima mjue tumaini la mwito wake.
Aleluya.
SHANGILIO
Mt.
13:31 – 35
Yesu
aliwatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na punje ya
haradali, aliyoitwaa mtu akaipanda katika shamba lake; nayo ni ndogo kuliko
mbegu zote; lakini ikiisha kumea, huwa kubwa kuliko mboga zote, ikawa mti, hata
nyuni wa angani huja na kukaa katika matawi yake.
Akawaambia
mfano mwingine; Ufalme wa mbinguni umefanana na chachu aliyoitwaa mwanamke,
akaisitiri ndani ya pishi tatu za unga, hata ukachachwa wote pia.
Hayo
yote Yesu aliwaambia makutano kwa mifano; wala pasipo mfano hakuwaambia neno;
ili litimie neno lililonenwa na nabii, akisema, Nitafumbua kinywa changu kwa
mifano, Nitayatamka yaliyositirika tangu awali.
Neno
la Bwana... Sifa kwako Ee Kristo.
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment