“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya Kila siku
Jumatatu, 19 Julai 2021
Juma la 16 la Mwaka
Kut 14:5-18
Kut 15:1-6 (K)1;
Mt 12:38-42
MKUBWA KULIKO YONA!
Kuna watu kati yetu ambao
hawajawahi kuwa na furaha, haijalisha unajitoa mara ngapi kwa ajili yao, daima
hawana furaha na wanalalamika daima. Licha ya mambo makuu ambayo Mungu ametenda
katika maisha yao, hawajawahi kuridhika. Wayahudi daima walitarajia muujiza
kutoka kwa nabii ili waweze kudhihirisha kama ni nabii wa kweli. Hawakumuamini
Yesu na wanaulizia ishara nyingi na miujiza ili waweze kumwamini. Lakini hata
kama Yesu angetenda muujiza mwingine wala isingeleta mabadiliko. Kwasababu
alivyo mponya yule kijana ambaye alikuwa kipofo (Mt12:22) walimshtumu kwa
kutenda miujiza kwa kutumia nguvu za Belzebul, mkuu wa pepo.
Yona alikuwa ishara.
Alikaa muda wa siku tatu ndani ya tumbo la nyangumi. Ni wazi kwamba walifahamu
kwamba amekufa. Lakini nyangumi alitumika kama chombo cha Mungu ili Yona aweze
kwenda Ninawi kwenda kuhubiri toba. Na kweli walitubu na kubadilisha maisha
yao. Giza ndani ya tumbo la nyangumi mwishoni, inabadilika na kuwa Baraka na
ishara kwa miaka iliyokuja. Habari ya Yona ilitoa ishara ya kifo cha Yesu, siku
tatu ndani ya kaburi na kufufuka kwake. Hii ndio ishara ambayo Yesu alikuwa
aitoe na anaendelea kuitoa. Ni ishara ya matumaini makubwa tukiichukulia
vizuri.
Lakini mara nyingi
tunaweza kuanguka katika majaribu makubwa. Ni mara nyingi pia tunataka ishara
zaidi ya ishara ambazo Yesu ameshatupatia. Tunataka uhakika mwingine kutoka kwa
Mungu kuhusu mapenzi yake. Tunataka yeye aongee kwa ufasaha na kwa sauti. Yesu
yupo nasi daima katika Ekaristi takatifu, akituponya kutoka katika magonjwa
yetu. Yesu Kristo yupo ndani ya jirani zetu tunaokutana nao. Ishara kuu ni
Mungu kuwa Mwanadamu na Neno kutwa mwili kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.
Yesu anatukumbusha sisi
kwamba tunapaswa kuamini kila kitu alicho ongea, hata kama tunajisikia tupo
katika giza kuu kama lile la tumbo la samaki au ndani ya kaburi, matumaini
hayajapotea. Mungu yupo katika vitu vyote na yupo kati yetu hata pale ambapo
tunaona yupo kimya. Anaongea nawe muda wote. Jifunze kuchagua mapenzi ya sauti
yake.
Sala: Bwana, naomba
unisaidie kukuamini wewe daima hata kama sioni miujiza na ishara kutoka
mbinguni. Nisaidie kukuamini hata katika wasi wasi na mashaka na udhaifu wangu
katika maisha. Ninaomba unipe Imani kamili katika kujibu wito wako katika
maisha yangu. Yesu anakuamini wewe. Amina
------------------------
Copyright ©2013-2020
©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment