“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya Kila siku
Ijumaa, 23 Julai, 2021,
Juma la 16 la Mwaka
Kut 20:1-17
Zab 19:8-11 (K) Yn 6:68;
Mt 13:18-18
MIZIZI ILIYOJIKITA KWA
KRISTO
Injili ya leo inatualika
kutafakari juu ya Yesu Kristo kama mpandaji wa neno la Mungu. Yesu anatualika
tulisikilize neno la Mungu na kuongozwa nalo katika maisha yetu. Kwa kufanya
hivyo mbegu iliyo pandwa mioyoni mwetu itazaa matunda. Mfano wa mpanzi
unaonesha nguvu ya Neno la Mungu kwa wale wote wanao lipokea kulisikiliza na
kulizamisha ndani mwao. Mfano wa mpanzi unawahusu wakristo wote hasa wale
wanaopaswa kuwalisha watu neno la Mungu kama vyombo vya Kristo.
Sisi tunaona wenyewe kati
yetu sisi wakristo wapo tunao jifananisha na zile mbegu zilizo anguka njiani,
mbegu zilizo anguka kwenye mwamba, na mbegu zilizo pandwa katika udongo mzuri.
Wakristo wote ambao hawajapandwa katika udongo mzuri ni wale ambao hawana
mizizi. Wanakiri Imani ya Kristo pale tu inapo pokelewa vizuri na watu, wakati
mambo ni marahisi. Lakini pale inapotoeka changamot katika kuhubiri Injili na
Neno la Mungu, na wakati maisha ya kumfuata Kristo hayana umaarufu, huyu mtu
huchagua njia nyingine ya tamaduni Fulani. Hili ni jambo la kweli kabisa katika
maisha yetu ya sasa.Tamaduni na ulimwengu vinapingana sana na ukweli wa Imani
ya Kristo. Ulimwengu unakuwa maarufu na tena wenye nguvu na kuonekana kama
sehemu ya ushindi. Matatizo ya kweli yanatokana na ukosefu wa Wakristo wengi
kukosa mizizi ya Imani katika maisha yao ya kila siku.
Cha muhimu kabisa ni
kuruhusu hili neno la Mungu lizamishwe ndani kabisa katika udongo wa roho zetu.
Hili linapo tokea neno linakuwa na kuwa imara. Na katika ulimwengu wa mawimbi
tukiwa kama wakristo tutashinda mawimbi na msuko suko wa dunia. Tutafakari kama
tupo tayari kusimama ndani ya Kristo au la. Tuombe Mungu azamishe mizizi ya
imani katika mioyo yetu ili tuweze kuwa imara bila kujali ina tugharimu nini.
Sala: Bwana, ninatamani
neno lako lizame kabisa katika moyo wangu. Ninatamani kubaki imara katika Imani
yangu bila kujali gharama. Ninatamani kuwa na Imani kubwa na katika upendo
wangu kwa kila kitu. Yesu, nakuamini wewe. Amina
------------------------
Copyright ©2013-2020
©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment