MASOMO YA MISA,
JUMATATU, JULAI 5, 2021
JUMA LA 14 LA MWAKA
SOMO 1
Mwa. 28:10-22
Yakobo alitoka
Beer-sheba, kwenda Harani. Akafika mahali fulanl akakaa huko usiku kucha, maana
jua lilikuwa limekuchwa; akatwaa jiwe moja la mahali pale akaliweka chini ya
kichwa chake, akalala usingizi pale pale.
Akaota ndoto; na tazama,
ngazi imesimamisha juu ya nchi, na ncha yake yafika mbinguni. Tena, tazama.
malaika wa Mungu wanapanda, na kushuka juu yake. Na tazama, Bwana amesimama juu
yake, akasema, Mimi ni Bwana, Mungu wa Ibrahimu baba yako, na Mungu wa Isaka;
nchi hii uilalayo nitakupa wewe na uzao wako. Na uzao wako utakuwa kama mavumbi
ya nchi, nawe utaenea upande wa magharibi, na mashariki, na kaskazini, na
kusini; na katika wewe, na katika uzao wako, jamaa zote za dunia watabarikiwa.
Na tazama, mimi nipo pamoja nawe, nitakulinda kila uendako, nami nitakuleta
tena mpaka nchi hii, kwa maana sitakuacha, hata nitakapokufanyia hayo
niliyokuambia.
Yakobo akaamka katika
usingizi wake, akasema, Kweli, Bwana yupo mahali hapa, wala mimi sikujua. Naye
akaogopa akasema, Mahali hapa panatisha kama nini! Bila shaka, hapa ni nyumba
ya Mungu, napo ndipo lango la mbinguni. Yakobo akaondoka asubuhi na mapema,
akalitwaa lile jiwe aliloliweka chini ya kichwa chake, akalisimamisha kama
nguzo, na kumimina mafuta juu yake. Akaita jina la mahali pale Betheli; lakini
jina la mji ule hapo kwanza uliitwa Luzu.
Yakobo akaweka nadhiri
akisema, Mungu akiwa pamoja nami, akinilinda katika njia niiendeayo, na kunipa
chakula nile, na nguo nivae; nami nikirudi kwa amani nyumbani kwa baba yangu,
ndipo Bwana atakuwa Mungu wangu. Na jiwe hili nililosimamisha kama nguzo
litakuwa nyumba ya Mungu; na katika kila utakalonipa hakika nitakutolea wewe
sehemu ya kumi.
Neno la Bwana… Tumshukuru
Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 91 :1-4, 14-15 (K) 2
(K) Mungu wangu
nitakayemtumaini.
Aketiye mahali pa siri
pake Aliye juu
Atakaa katika uvuli wake
Mwenyezi.
Nitasema, Bwana ndiye
kimbilio langu na ngome yangu,
Mungu wangu
nitakayemtumaini. (K)
Maana Yeye atakuokoa na
mtego wa mwindaji,
Na katika tauni iharibuyo.
Kwa manyoya yake
atakufunika,
Chini ya mbawa zake
utapata kimbilio;
Uaminifu wake ni ngao na
kigao. (K)
Kwa kuwa amekaza
kunipenda
Nitamwokoa; na kumweka
palipo juu,
Kwa kuwa amenijua jina
langu.
Ataniita nami
nilamwitikia;
NitaKuwa pamoja naye
taabuni,
Nitamwokoa na kumtukuza.
(K)
SHANGILIO
Lk.8:15
Aleluya, aleluya,
Wanabarikiwa wale ambao
kwa unyofu
na wema wa mioyo yao,
hulisikia neno la Mungu
na kulishika.
Aleluya.
INJILI
Mt. 9: 18-26
Yesu alipokuwa akiwaambia
hayo, tazama, akaja jumbe mmoja, akamsujudia, akisema, Binti yangu sasa hivi
amekufa; lakini njoo, uweke mkono wako juu yake, naye ataishi. Akaondoka Yesu,
akamfuata, pamoja na wanafunzi wake.
Na tazama, mwanamke
aliyekuwa na ugonjwa wa kutoka damu muda wa miaka kumi na miwili, alikuja kwa
nyuma, akaugusa upindo wa vazi lake. Kwa maana alisema moyoni mwake, Nikigusa
tu upindo wa vazi lake nitapona. Yesu akageuka, akamwona, akamwambia, Jipe moyo
mkuu, binti yangu, imani yako imekuponya. Yule mwanamke akapona tangu saa ile.
Yesu alipofika nyumbani
kwa yule jumbe, aliona wapiga filimbi, na makutano wakifanya maombolezo,
akawaambia, Ondokeni; kwa maana kijana hakufa, amelala tu. Wakamcheka sana.
Lakini makutano walipoondoshwa, aliingia, akamshika mkono; yule kijana
akasimama. Zikaenea habari hizi katika nchi ile yote.
Neno la Bwana........Sifa
kwako Ee Kristo
Copyright © 2020,
"MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora –
Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see
www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment