"ASALI ITOKAYO
MWAMBANI"
Tafakari ya kila siku
Jumatatu, Julai 5, 2021.
Juma la 14 la Mwaka
Mwa 28:10-22;
Zab 90:1-4, 14-15;
Mt 9:18-26
IMANI NA UPONYAJI
Leo katika Injili,
tunaona matukio mawili ya miujiza wa kuponya. Hawa ni watu walio muhitaji Yesu
ili waponye. Tunakutana na watu wengi wanao ulizia kuhusu upendo wa Mungu na
kwanini Mungu hawaponyi? Kuna wengine pia wanajiuliza pia kuhusu Imani yao
wenyewe wanajisikia kama wangekuwa na Imani kubwa zaidi kwa Mungu ungekuta
Mungu amesha waponya.
Kijana mmoja aliitwa
Stefano wa umri wa miaka 18, alipata ajali ya gari na alipata hitilafu katika
ubongo wake kiasi cha kushindwa pia kuongea vizuri. Na mwaka mmoja baadaye
akadondoka kutoka kwenye paa la nyumba, akapooza kuanzia kwenye kiuno kushuka
chini. Daktari akamwambia Stefano hutaweze kutembea tena. Lakini Stefano
akamwambia Mungu ameniambia huu ni muda wake wakuniponya. Imani yake ilikuwa ya
kweli na hakika, hakuwa na mashaka yeyote kwamba Mungu atamponya. Siku moja
watu walikusanyika kumuombea, yeye alienda mbele kwakujivuta na kukaa mbele
yao, wakamuombea na kusali sana lakini hali yake ikabaki vile vile. Baada ya
hapo watu walimuhuzunikia sana kwa hali yake. Walishangaa sana kwamba alikuwa
na Imani na walijiridhisha kwamba atapona lakini wakashnga sasa Imani yake
imekuwaje tena? Baada ya mkutano wao wakamkuta Stefano wakashngaa. Alikuwa
hayupo vizuri lakini Imani yake ilikuwa haijayumbishwa. Kwa sauti ya huzuni
Stefano alisema “haikuwa muda wangu wakupona lakini siku moja nitasimama na
kukimbia”.
Hakika tuna muujiza hapa.
Muujiza haukuwa katika miguu yake, bali ulikuwa muujiza wa roho yake. Mwanga wa
Yesu ulikuwa ukingaa ndani ya roho yake. Na zaidi ya yote, uponyaji wa mwili ni
kwaajili ya muda mfupi. Bali uponyaji wa roho na Uponyaji wa Imani unadumu kwaajili
ya uzima wa milele. Tumuombe Mungu atusaidie kushughulika zaidi na uponyaji wa
Imani yetu na maisha yetu ya kiroho ili tuweze kupata nafasi katika maisha ya
milele.
Je, unatambua kina cha
nguvu ya Yesu? Je, unatambua upendo wake unamsukuma atumie nguvu yake kwa ajili
ya uzuri wako? Kutambua na kukubali ukweli huu utabadilisha maisha yako na
kumruhusu yeye afanye miujiza ya Imani.
Sala: Bwana, ninaamini
juu ya nguvu zako kamili juu ya vitu vyote na mamlaka yote kuhusu maisha yangu.
Nisaidie mimi nikuamini wewe na kuamini juu ya upendo wangu kwako. Amina
------------------------
Copyright ©2013-2020
©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment