MASOMO YA MISA, JULAI 9,
2021
IJUMAA, JUMA LA 14 LA
MWAKA
SOMO 1
Mwa. 46:1-7, 28-30
Israeli alisafiri pamoja
na yote aliyokuwa nayo, akaja Beer-sheba, akamchinjia sadaka Mungu wa Isaka
babaye. Mungu akanena na Israeli katika ndoto ya usiku, akasema, Yakobo,
Yakobo. Akasema, Mimi hapa. Akasema, Mimi ni Mungu, Mungu wa baba yako,
usiogope kushuka mpaka Misri; maana nitakufanya uwe taifa kubwa huko. Mimi
nitashuka pamoja nawe mpaka Misri; nami nitakupandisha tena bila shaka; na
yusufu ataweka mkono wake juu ya macho yako. Yakobo akaondoka kutoka
Beer-sheba; wana wa Israeli wakamchukua baba yao, na watoto wao wadogo, na wake
zao katika magari aliyoyapeleka Farao ili kumchukua.
Wakatwaa na wanyama wao,
na mali zao walizokuwa wamezipata katika nchi ya Kanaani, wakaja Misri, Yakobo
na uzao wake wote pamoja naye. Wanawe, na wana wa wanawe, pamoja naye, binti
zake nab inti za wanawe, na uzao wake wote, aliwaleta pamoja naye mpka Misri.
Yakobo akampeleka Yuda
mbele yake kwa Yusufu, ili amwongoze njia mpaka Gosheni. Wakaja mpaka nchi ya
Gosheni. Yusufu akatandika gari lake, akapanda kwenda kumlaki Israeli babaye,
huko Gosheni; akajionyesha kwake, akamwangukia shingoni, akalia shingoni mwake,
kitambo kizima. Israeli akamwambia Yusufu, na nife sasa, kwa kuwa nimekuona uso
wako, ya kuwa ungali hai.
Neno la Bwana… Tumshukuru
Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 37:3-4, 6 – 7,
18-19, 27-28, 39-40 (K) 39
(K) Wokovu wa wenye haki
una Bwana.
Umtumaini Bwana ukatende
mema,
Ukae katika nchi,
ukapendezwe na uaminifu.
Nawe utajifurahisha kwa
Bwana,
Naye atakupa haja za moyo
wako. (K)
Bwana anazijua siku za
wakamilifu,
Na urithi wao utakuwa wa
milele.
Hawataaibika wakati wa
ubaya,
Na siku za njaa
watashiba. (K)
Jiepue na uovu, utende
mema,
Na kukaa hata milele.
Kwa kuwa Bwana hupenda
haki,
Wala hawaachi watauwa
wake. (K)
Na wokovu wenye haki una
Bwana,
Yeye ni ngome yao wakati
wa taabu.
Naye Bwana huwasaidia na
kuwaopoa,
Huwaopoa na wasio haki na
kuwaokoa,
Kwa kuwa wamemtumaini
Yeye. (K)
SHANGILIO
Yak. 1:21
Aleluya, aleluya,
Pokeeni kwa upole neno la
Mungu lililopandwa ndani, liwezalo kuziokoa roho zenu.
Aleluya.
INJILI
Mt. 10: 16 – 23
Yesu aliwaambia mitume
wake: Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwa mwitu; basi iweni na
busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua.
Jihadharini na wanadamu;
kwa maana watawapeleka mabarazani, na katika masinagogi yao watawapiga; nanyi
mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao
na kwa mataifa. Lakini hapo watakapowapeleka, msifikirifikiri jinsi
mtakavyosema; maana mtapewa saa ile mtakayosema. Kwa kuwa si ninyi msemao, bali
ni Roho wa Baba yenu ndani yenu.
Na ndugu atamsaliti
nduguye ili auawe, na baba atamsaliti mwana, na wana watawainukia wazazi wao,
na kuwafisha. Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu;
lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka. Lakini
watakapowafukuza katika mji huu, kimbilieni mwingine; kwa maana ni kweli
nawaambia, Hamtaimaliza miji ya Israeli, hata ajapo Mwana wa Adamu.
Neno la Bwana… Sifa kwako
Ee Kristo.
Copyright © 2020,
"MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora –
Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see
www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment