MASOMO YA MISA, JULAI 20,
2021
JUMANNE , JUMA LA 16 LA
MWAKA
SOMO 1
Kut. 14:21-15:1
Musa alinyosha mkono wake
juu ya bahari; Bwana akaifanya bahari irudi nyuma kwa upepo wa nguvu utokao
mashariki, usiku kucha, akaifanya bahari kuwa nchi kavu, maji yakagawanyika
Wana wa Israeli wakaenda ndani kati ya bahari katika nchi kavu; nayo maji yalikuwa
ukuta kwao mono wa kuume, na mkono wa kushoto.
Na wale Wamisri
wakawafuatia, wakaingia ndani kati ya bahari, farasi zote za Farao, na magari
yake, na wapanda farasi wake. Ikawa katika zamu ya alfajiri, Bwana
akalichungulia jeshi la Wamisri katika ile nguzo ya moto na ya wingu,
akalifadhaisha jeshi la Wamisri. Akayaondoa magurudumu ya magari yao, hata
yakaenda kwa uzito; na Wamisri wakasema, Na tukimbie mbele ya Israeli; kwa kuwa
Bwana anawapigania, kinyume cha Wamisri.
Bwana akamwambia Musa,
Nyosha mkono wako juu ya bahari, ili maji yarudi tena juu ya Wamisri, juu ya
magari yao, na juu ya farasi zao. Musa akaunyosha mkoon wake juu ya bahari, na
kulippambazuka, bahari ikarudi kwa nguvu zake; Wamisri wakakimbia mbele yake;
na Bwana akawakukutia mbali hao Wamisri kati ya bahari. Yale maji yakarudi
yakafunikiza magari na wapanda farasi, hata jeshi lote la Farao lililoingia
katika bahari nyuma yao; hakusalia hata mtu mmoja. Lakini wana wa Israeli
wakaenda katika nchi kavu katikati ya bahari; na hayo maji yalikuwa ni makuta
upande wao wa kuume, na upande wao wa kushoto.
Ndivyo Bwana alivyowaokoa
Israeli siku ile mikononi mwa Wamisri; Waisraeli wakawaona Wamisri ufuoni kwa
bahari, wamekufa. Israeli akaiona ile kazi kubwa aliyoifanya Bwana juu ya
Wamisri, ndipo hao watu wakamcha Bwana, wakamwamini Bwana, na Musa mtumishi
wake.
Ndipo Musa na wana wa
Israeli wakamwimbia Bwana wimbo huu wakanena, na kusema, Nitamwimbia Bwana, kwa
maana ametukuka sana; Farasi na mpanda farasi amewatupa baharini.
Neno la Bwana... Tumshukuru
Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 15:8-10, 12, 17 (K)
1
(K) Nitamwimbia Bwana,
kwa maana ametukuka sana..
Kwa upepo wa mianzi ya
pua yako maji yalipandishwa,
Mawimbi yakasimama juu
wima mfano wa chungu,
Vilindi vikagandamana
ndani ya moyo wa bahari.
Adui akasema Nitafuatia,
nitapata nitagawanya nyara,
Nafsi yangu itashibishwa
na wao;
Nitaufuta upanga wangu,
Mkono wangu
utawaangamiza. (K)
Ulinyosha mkono wako wa
kuume,
Nchi ikawameza.
Ulivuma kwa upepo wako,
bahari ikawafunikiza;
Wakazama kama risasi
ndani ya maji makuu. (K)
Utawaingiza, na kuwapanda
Katika mlima wa urithi
wako,
Mahali pale
ulipojifanyia, Ee Bwana, ili upakae,
Pale patakatifu
ulipopaweka imara, Bwana,
Kwa mikono yako. (K)
SHANGILIO
Zab. 130:5
Aleluya, aleluya,
Roho yangu inamngoja Bwana,
na neno lake nimelitumainia.
Aleluya.
INJILI
Mt. 12:46 – 50
Yesu alipokuwa katika
kusema na makutano, tazama, mama yake na ndugu zake walikuwa wakisimama nje
wataka kusema naye. Mtu mmoja akamwambia, Tazama, mama yako na ndugu zako
wamesimama nje, wanataka kusema nawe. Akajibu, akamwambia yule aliyempasha
habari, Mama yangu ni nani? Na ndugu zangu ni akina nani? Akawanyoshea mkono
wanafunzi wake, akasema, Tazama, Mama yangu na ndugu zangu! Kwa maana yeyote
atakayeyafanya mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni, huyu ndiye ndugu yangu, na
umbu langu, na mama yangu.
Neno la Bwana... Sifa
kwako Ee Kristo.
Copyright © 2020,
"MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora –
Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment