“ASALI ITOKAYO MWMABANI”
Tafakari ya kila Siku
Alhamisi, Julai 22, 2021.
Juma la 15 la Mwaka
Sikukuu ya Mt. Maria
Magdalena
Wimbo 3:1-4 or 2Cor
5:14-17;
Zab 63: 1-5, 7-8;
Yn 20:1-2, 11-18.
KUZAMA KATIKA KRISTO!
*Mungu aweza badili
Historia yako na kuwa Bora zaidi*
Karibuni ndugu wapendwa
kwa adhimisho la misa takatifu asubuhi ya leo. Bwana ametuchagua tangu tumboni
mwa mama zetu, ametupatia nguvu, baraka na neema na kila kifaachi kwa ajili ya
kuendesha uwepo wetu hapa duniani. Magumu na dhoruba zitajitokeza lakini katika
kila dhoruba, ipo nguvu na neema ya kushindana na dhoruba hizo. Hivyo,
tunapaswa kujipa moyo ili tuweze kuziona nguvu za neema hiyo. Mungu ana mipango
bora na kila mmoja wetu. Ndivyo ilivyotokea kwa Maria Magdalena. Mungu ana
mpango na kila mmoja wetu. Yeye atupatiapo utume, hakika anatupatia na nguvu za
kuutekeleza pia.
Alimmiminia neema hizo
Mt. Maria Magdalena, yeye alikuwa na pepo wengi, waliokuwa kikwazo kwake katika
kuifanya kazi ya Bwana. Lakini aliweza kutakaswa na Bwana na kuwa kiumbe cha
kutangaza habari za Kristo mfufuka. Aliweza kuwa mtume kwa mitume wa Yesu, Yeye
alitumwa na Yesu kuwapasha habari mitume kwamba Yesu amefufuka. Sisi nasi
tukimtegemea Bwana, hakika atatubadilisha na kutufanya tutende mambo bora
zaidi. Tusitumie historia zetu mbaya kujihukumu, tumtegemee Bwana na hakika aweza
kugeuza historia zetu na kuwa historia bora na za mafanikio. Tumtegemee Yesu;
amewabadilisha wengi, atatubadiisha na sisi pia.
Tumuombe Mt. Maria
Magdalena, atuombee tupate ujasiri wa kubadili historia dhaifu za maisha yetu
na kuwa historia zenye kuniletea mafanikio zaidi.
------------------------
Copyright ©2013-2020
©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment