“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Jumatano, Juni 9, 2021
Juma la 10 la Mwaka
2 Kor 3: 4-11;
Zab 99: 5-9;
Mt 5: 17-19.
SHERIA YA UPENDO!
Katika Injili ya leo,
Yesu kwa hakika anawahakikishia wanaomsikiliza kwamba, “Sikuja kutengua sheria
na manabii. Nimekuja si kutengua bali kuikamilisha”. Yesu alikuja si kuifuta
sheria bali aiinue katika hali ya juu ya ukamilifu. Mtazamo wa Yesu unatusaidia
tuione sheria katika mwanga mpya. Maneno yake ni kwa ajili ya kufariji lakini
pia yanaleta changamoto, akionesha njia inayoenda juu sana kuliko sheria mpaka
kwenye sheria ya Upendo. Sheria isiyo na upendo haiwezi kulinda utu na maisha
ya mwanadamu. Inamfanya mwanadamu awe kama aina fulani ya kitu kisicho na uhai.
Yesu anatutaka tuwe na upendo zaidi. Pengine wakati mwingine tunasisitiza mno
sheria kiasi cha kushindwa kuonesha upendo na msamaha kwa wengine.
Tuwatazame watu walio
wekwa na Mungu mbele yetu ili tuwapende. Hili ni kwa ajili pia ya ndugu zetu
katika familia lakini pia katika wana ndoa. Je, ni mara ngapi tunavyokuwa
makini kwa kitendo kidogo cha huruma na upendo?. Je tunatafuta muda wa kutumia
maneno ya kutia moyo? Je, tunatumia jitihada hata kuwaonesha kwamba tunawajali?
Upendo upo katika utukufu na utukufu huu unaonesha kushika amri ya Mungu ya
mapendo.
Katika maisha yetu,
tunapaswa kuwa tayari kusonga mbele tukiwa wabunifu wa njia mpya za kuweza
kutufanya tuelewe na kuishi Imani yetu zaidi. Tamaduni zetu na mapokeo yetu ni
mazuri na tusiyapoteze lakini pia tutumie hali hiyo hiyo katika kuelewa na
kuangalia hitaji la sasa.
Sala: Bwana, nisaidie
niweze kuwa makini kwa njia kubwa na katika njia ndogo ndogo unazo niita ili
kukupenda wewe na jirani. Nisaidie hasa, niweze kuangalia muda hata mdogo
nioneshe upendo na hivyo kutimiza sheria yako. Yesu nakuamini wewe. Amina.
------------------------
Copyright ©2013-2020
©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment