MASOMO YA MISA, JUNI 9 2021
JUMATANO, JUMA LA 10 LA
MWAKA
SOMO 1
2Kor. 3:4-11
Tumaini hilo tunalo mbele
za Mungu kwa njia ya Kristo. Si kwamba twatosha sisi wenyewe kufikiri neno
lolote kwamba ni letu wenyewe, bali utoshelevu wetu watoka kwa Mungu. Naye
ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko bali war oho;
kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha. Basi, ikiwa huduma ya mauti
iliyoandikwa na kuchorwa katika mawe, ilikuja katika utukufu, hata Waisraeli
hawakuweza kuukazia macho uso wa Musa, kwa sababu ya utukufu wa uso wake; nao
ni utukufu uliokuwa ukibatilika; je! Huduma ya roho haitazidi kuwa katika
utukufu? Kwa maana ikiwa huduma ya adhabu ina utukufu, siuze huduma ya haki ina
utukufu unaozidi. Maana hata ile iliyotukuzwa haikuwa na utukufu hivi, kwa sababu
ya utukufu uzidio sana. Kwa maana, ikiwa ile inayobatilika ilikuwa na utukufu,
zaidi sana ile ikaayo ina utukufu.
Neno la Bwana… Tumshukuru
Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 99:5-9 (K) 9
(K) Bwana, Mungu wetu,
ndiye mtakatifu.
Mtukuzeni Bwana, Mungu
wetu;
Sujuduni penye kiti cha
miguu yake;
Ndiye mtakatifu. (K)
Musa na Haurni miongoni
mwa makuhani wake,
Na Samweli miongoni mwao
waliitiao jina lake,
Walipomwita Bwana
aliwaitikia. (K)
Katika nguzo ya wingi
alikuwa akisema nao.
Walishika shuhuda zake na
amri aliyowapa. (K)
Ee Bwana, Mungu wetu,
ndiwe uliyewajibu;
Ulikuwa kwao Mungu mwenye
kusamehe
Ingawa uliwapatiliza
matendo yao. (K)
Mtukuzeni Bwana, Mungu
wetu;
Sujuduni mkiukabili mlima
wake mtakatifu;
Maana Bwana, Mungu wetu,
ndiye mtakatifu. (K)
SHANGILIO
Zab. 119:135
Aleluya, aleluya,
Umwangazie mtumishi wako
uso wako, na kunifundisha amri zako.
Aleluya.
INJILI
Mt. 5:17-19
Yesu aliwaambia wanafunzi
wake: Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja
kutangua, bali kutimiliza. Kwa maana, amin, nawaambia, mpaka mbingu nan chi
zitakapoondoka, yodi moja wala nukata moja ya torati haitaondoka, hata yote
yatimie. Basi mtu yeyote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na
kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali
mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa
mbinguni.
Neno la Bwana… Sifa kwako
Ee Kristo.
-------------------------
Copyright © 2020,
"MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora –
Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see
www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment