“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Jumamosi, Juni 5, 2021.
Juma la 9 la Mwaka
Jumamosi kumbukumbu ya
Bikira Maria.
Tob 12:1, 5-15, 20;
Tob 13:2, 6-8;
Mk 12: 38-44.
MKARIMU KAMA MJANE
MASKINI!
Somo la Injili linatoa
picha Yesu akiwa na wafuasi wake, akiwa amekaa akiangalia watu wakiwa wanatoa
sadaka hekaluni. Wale watu waliopenda kuonekana kuwa watu wa karimu walitoa
nyingi sana. Lakini tazama anatokea mjane maskini, ambaye katika hali ya ukimya
na unyofu anaweka senti mbili. Yesu mara moja anavutwa na kitendo hichi na
anawaambia wafuasi wake. Aliweka senti mbili tu kiasi ambacho kilikuwa ni
kidogo sana. Lakini tazama Yesu anamtangaza kwamba ametoa nyingi zaidi kuliko
wengine. Yesu anaelezea tofauti juu ya utajiri wa kimwili na utajiri wa kiroho.
Utajiri wa kiroho na ukarimu wa kiroho ni muhimu zaidi kuliko utajiri wa
kimwili. Mjane huyu alikuwa maskini kimwili lakini alikuwa tajiri kiroho. Wale
waliokuwa na kiasi kikubwa cha fedha walionekana kuwa matajiri wa kimwili
lakini maskini wa kiroho kuliko mjane huyu.
Katika ulimwengu wa
kutafuta mali tunaoishi katika, ni vigumu kuamini. Ni vigumu kugeuza dhamiri na
kugeukia utajiri wa kiroho wenye Baraka nyingi. Tunapaswa kuwa kama huyu mjane
maskini na kutoa yote tulionayo. Alitaka kuleta tofauti. Alitoa yote aliokuwa
nayo.
Kila mtu anapaswa
kuangalia ni kwa jinsi ghani hili linaingia katika maisha yake. Tunapaswa kuwa
na hali ya ndani ya kuwa na ukarimu na hali ya kuachia. Kuanzia hapa, Bwana
atakuonesha ni kwa jinsi ghani ya kutumia mali zetu kwa ajili ya faida ya uzuri
wetu na kwa ajili ya wengine pia. Toa ulionayo na jinsi ulivyo kwake, naye
ataelekeza moyo wako kadiri ya utukufu wake mkamilifu.
Sala: Bwana, ninaomba
unipe moyo wa ukarimu na uondoe moyo wa ubinafsi kama yule mjane. Nisaidie mimi
nitafute njia za kujitoa kabisa kwako, bila kushikilia mambo mengine nyuma
yangu, na zaidi kutafuta utukufu wa kiroho katika ufalme wako. Yesu, nakuamini
wewe. Amina.
------------------------
Copyright ©2013-2020
©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment