MASOMO YA MISA, JUNI 8,
2021
JUMANNE, JUMA LA 10 LA
MWAKA
KUMBUKUMBU YA MT. ANTONI
WA PADUA
SOMO 1
2Kor. 1:18 – 22
Kama Mungu alivyo
mwaminifu, neno letu kwenu si Nidyo na siyo. Maana Mwana wa Mungu, Kristo Yesu,
aliyehubiriwa katikati yenu na sisi, mimi na Silwano na Timotheo, hakuwa Ndiyo
na siyo; bali katika yeye ni Ndiyo. Maana ahadi zote za Mungu zilizopo katika
yeye ni Ndiyo; tena kwa hiyo katika yeye ni Amin; Mungu apate kutukuzwa kwa
sisi. Basi Yeye atufanyaye imara pamoja nanyi katika Krito, na kututia mafuta,
ni Mungu, naye ndiye aliyetutia muhuri akatupa arabuni ya Roho mioyoni mwetu.
Neno la Bwana… Tumshukuru
Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 119:129 – 133, 135
(K) 135
(K) Umwangazie mtumishi
wako uso wako.
Shuhuda zako ni za ajabu,
Ndiyo maana roho yangu
imezishika.
Kufafanusha maneno yako
kwatia nuru,
Na kumfahamisha mjinga.
(K)
Nalifunua kinywa changu
nikatweta,
Maana naliyatamani
maagizo yako.
Unigeukie, unirehemu
mimi,
Kama iwahusuvyo
walipendao jina lako. (K)
Uzielekeze hatua zangu
kwa neno lako,
Uovu usije ukanimiliki.
Umwangazie mtumishi wako
uso wako,
Na kunifundisha amri
zako. (K)
SHANGILIO
Zab. 19:18
Aleluya, aleluya.
Amri ya Bwana ni safi,
huyatia macho nuru.
Aleluya.
INJILI
Yesu aliwaambia wanafunzi
wake: Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini
hata ikolee? Haifai tena kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu. Ninyi
ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima. Wala watu
hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza
wote waliomo nyumbani. Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate
kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.
Neno la Bwana… Sifa kwako
Ee Kristo.
-------------------------
Copyright © 2020,
"MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora –
Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see
www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment