ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya Kila siku
Jumanne, Juni 8, 2021,
Juma la 10 la Mwaka
Kumbukumbu ya Mt. Antoni
wa Padua
2 Kor 1: 18-22;
Zab 119: 129-133, 135;
Mt 5: 13-16
CHUMVI NA MWANGA
Yesu anawaambia Wafuasi
wake: ninyi ni chumvi ya ulimwengu. Ninyi ni mwanga wa ulimwengu. Maneno haya
ni utangulizi wa maneno ambayo Yesu atayasema katika hutuba ya mlimani. Wafuasi
wa Yesu wanatakiwa maneno ya Yesu yapenye ndani yao, ya watawale na wayaishi.
Katika Agano la Kale,
WaisraelI walipewa Amri kumi na Agano likafanywa kati yao likiwataka waishi
kitakatifu na kwa haki kama wanavyotakiwa na Agano. Je, walitambua wao ni
chumvi ya ulimwengu?. Walisisitiza sana kuhusu sheria, mpaka wakaua ile roho. Yesu
anaonesha hili kwa wafuasi wake kwakuwaambia, wema wao usipozama ndani
nakuushinda ule wa Walimu wa sheria na Mafarisayo, hawawezi kuwa chumvi ya
ulimwengu. Yesu aliwataka Wafuasi wake wawe chumvi ya ulimwengu, si kwakusimama
na kuonekana kama watakatifu machoni pa watu bali kwa maadili mema na utu ambao
umevishwa taji ya upendo kwa Mungu na kwa jirani. Kwa wema, maadili na utu huu
uliovishwa taji, na kungarishwa na Imani, matumaini na mapendo, wakristo
wanaalikwa kuwa mwanga wa Ulimwengu. Hawahitaji kujitangaza kwamba wao ni
Wakristu. Wataonesha kwamba wao ni Wakristo “kwanjia hii wote watajua ya kuwa
ninyi ni wafuasi wangu, kama mna pendana ninyi kwa ninyi” (Yn 13: 35).
Kama tunavyoweza kufikiri
mlo bila chumvi, au kupotelea msituni wakati wa usiku, tutatambua ni kitu ghani
Yesu anatuambia. Kiasi kidogo cha chumvi au kiasi kidogo cha mwanga kina badili
kila kitu. Mt. Fransisko wa Assis anatuambia giza lote la ulimwengu mzima
haliwezi kuzima hata mwanga wa mshumaa mmoja. Ulimwengu tunaoishi upo gizani katika
hali mbali mbali. Mungu anatuita mimi na wewe tuweze kuwa chumvi na mwanga na
kuwaonesha watu njia. Mungu anataka kungara kupitia wewe na mimi, na anakutaka
wewe uangaze. Jukumu letu ni kuwa wawazi.
Sala: Bwana, ninataka
kutumiwa na wewe. Ninataka kuwa chumvi na mwanga. Ninataka kufanya mabadiliko
ulimwenguni. Ninajitoa kwako kwa huduma yako. Yesu, ninakuamini wewe. Amina.
------------------------
Copyright ©2013-2020
©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment