MASOMO YA MISA JUNI 4,
2021
IJUMAA, JUMA LA 9 LA
MWAKA
SOMO 1
Tob. 11:5-15
Ana alikuwa amekaa
kuyaelekeza macho yake njiani hali akimtazamia mwanawe. Akamwona mbwa akija
mbio; akamwambia mumewe, Lo-o-o! Mwanao anakuja, na yule mtu aliyefuatana naye.
Rafaeli akamwambia Tobia,
Najua ya kuwa baba yako atafumbua macho yake. Basi umtie mara nyongo machoni;
na imchomapo atajifikicha; na vyamba vyeupe vitaambuka; atakuona kwa macho.
Lakini Ana alimkimbilia,
akamwangukia mwanawe shingoni, akamwambia, Mwanangu! Nimekuona; tangu sasa ni
radhi nife. Wakalia wote wawili. Tobiti naye akaondoka kwenda mlangoni,
akajikwaa; lakini mwanawe akamkimbilia, akamshika baba yake; akamtia nyongo machoni,
akasema, Jipe moyo, baba yangu. Yeye macho yake yalipoanza kuwasha
aliyefikicha; navyo vyamba vyeupe vikaambuka katika pembe za macho yake,
akamwona mwanawe, akamwangukia shingoni. Akalia, akasema, Ee Mungu umehimidiwa;
na jina lako limehimidiwa milele; na watukuzwe malaika zako watakatifu wote.
Kwa maana umenirudi, ukanihurumia; lo-o—o; namwona mwanangu Tobia.
Neno la Bwana...
Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 145:1,7-10 (K)
(K) Ee nafsi yangu,
umsifu Bwana.
Au: Aleluya.
Aleluya.
Ee nafsi yangu, umsifu
Bwana.
Nitamsifu Bwana muda
ninaoishi,
Nitamwimbia Mungu wangu
ningali ni hai. (K)
Huishika kweli milele,
Huwafanyia hukumu
walioonewa.
Huwapa wenye njaa
chakula;
Bwana hufungua
waliofungwa. (K)
Bwana huwafumbua macho
waliopofuka;
Bwana huwainua
walioinama;
Bwana huwapenda wenye
haki;
Bwana huwahifadhi wageni;
Huwategemeza yatima na
mjane. (K)
Bwana atamiliki milele,
Mungu wako, ee Sayuni,
Kizazi hata kizazi. (K)
SHANGILIO
Zab. 111 :7, 8
Aleluya, aleluya,
Unitie nguvu sawasawa na
neno lako, ee Bwana, unifundishe njia ya amri zako.
Aleluya.
INJILI
Mk. 12:35-37
Yesu alipokuwa
akifundisha katika hekalu, alijibu, akasema, Husemaje waandishi ya kwamba
Kristo ni Mwana wa Daudi? Daudi mwenyewe alisema, kwa uweza wa Roho Mtakatifu.
Bwana alimwambia Bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kuume, hata niwawekapo adui
zako kuwa chini ya miguu yako. Daudi mwenyewe asema ni Bwana; basi amekuwaje
mwanawe? Na mkutano mkubwa walikuwa wakimsikiliza kwa furaha.
Neno la Bwana... Sifa
kwako Ee Kristo.
-------------------------
Copyright © 2020,
"MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora –
Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see
www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment