“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Ijumaa, Juni 4, 2021,
Juma la 9 la Mwaka
Tob 11:5-17;
Zab 145:2, 7-10;
Mk 12: 35-37.
FURAHIA NDANI YA BWANA!
Sisi Wakristo tunafahamu
kwamba Yesu ni Masiha, Mwana wa Daudi. “Mwana wa Daudi” jina linalo mwakilisha
Yesu huku likitengeneza uti wa mgongo wa Injili. Katika Maamkio ya Bikira Maria
alipokea ujumbe huu “Na Bwana Mungu atampa kiti cha Daudi Baba yake, na atatawala
nyumba ya Yakobo milele, na Ufalme wake hautakuwa na Mwisho” (Lk 1:32-33). Yule
Maskini aliyekuwa mwombaji alimwomba Yesu amponye, akisema “Yesu Mwana wa
Daudi, unihurumie mimi” (Mk 10:48). Wakati Yesu alivyokuwa akiingia Yerusalemu
walimshangilia wakisema “Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana, hosanna juu
mbinguni” (Mk 11:10).
Lakini sio tu Mwana wa
Daudi, yeye pia ni Bwana. Analionesha hili yeye mwenyewe kwa kunukuu zaburi ya
Daudi 110. Mt. Petro, aliye shahidi wa ufufuko wa Bwana, aliona wazi kwamba
Yesu amethibitiswa “Bwana wa Daudi”, kwasababu “ndugu zangu nina waambia kwa
ujasiri kwamba Babu yetu Daudi alikufa na akazikwa na kaburi lake lipo hapa
hadi leo…lakini Yesu ambaye ni Mungu alifufuka, ambao sisi ni mashahidi wake.”
(Mdo 2:29-32).
Leo Yesu anajaribu
kuwaelewesha Wayahudi kuhusu Masiha au Kristo. Masiha atakuwa Daudi mpya,
akitawala juu ya Ufalme wake, lakini atatawala milele katika ufalme wa milele,
kama Malaika Garieli alivyo tangaza kwa Maria (Lk 1:32-33; Is 9:7). Atakuwa
Mwana wa Mungu kwa asili, na hivyo atakuwa Mungu mwenyewe, mwenye Umungu sawa
na Baba.
“Umati mkubwa walisikia
hili kwa shauku na furaha (Mark 12:37). Mafundisho ya Yesu yalileta furaha sana
katika mioyo yao. “Je, mimi nina yarufahia maneno ya Yesu?” ni mara nyingi tunayaona
maneno ya Yesu kama mzigo, au kuwa kikwazo kwa mambo ambayo tunataka kufanya
katika maisha. Furaha katika Bwana ni kitu ambacho kinatufanya kukuwa zaidi
kila siku. Tujiruhusu kufurahi katika Bwana na kufurahia uwepo wa maneno yake.
Tukiwa “tumeiva vizuri” tutamtafuta yeye zaidi.
Sala: Bwana Yesu, Mwana
wa Daudi, ninatamani kufurahia katika wewe. Nisaidie niweze kuacha mambo yote
ya ulimwengu yanayo niweka mbali nawe. Nisaidie niweze kukutafuta wewe na neno
lako daima. Jaza roho yangu na furaha yako. Yesu, nakuamini wewe. Amina.
------------------------
Copyright ©2013-2020
©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment