MASOMO YA MISA, JUNI 29,
2021
JUMANNE, JUMA LA 12 LA MWAKA
SHEREHE YA WATAKATIFU
PETRO NA PAULO (MITUME)
SOMO 1
Mdo. 12:1 – 11
Herode mfalme alinyosha
mikono yake kuwatenda mabaya baadhi ya watu wa kanisa. Akamwua Yakobo, ndugu
yake Yohane, kwa upanga. Na akiona ya kuwa imewapendenza Wayahudi akaendelea
akamshika na Petro. Siku hizo zilikuwa siku za mikate isiyochachwa. Alipokwisha
kumkamata, akamweka gerezani akamtia mikononi mwa vikosi vinne vya askari wanne
wanne, wamlinde, akitaka baada ya Pasaka kumtoa na kumweka mbele ya watu. Basi
Petro akalindwa gerezani, nalo kanisa likamwomba Mungu kwa juhudi kwa ajili
yake.
Hata wakati Herode
alipotaka kumtoa, usiku ule ule Petro alikuwa amelala katikati ya askari
wawili, amefungwa minyororo miwili; walinzi mbele ya mlango wakailinda gereza.
Mara malaika wa Bwana akasimama karibu naye, nuru ikamulika mle chumbani
akampiga Petro ubavuni, akamwamsha, akisema, Ondoka upesi. Minyororo yake
ikamwangukia mikononi. Malaika akamwambia, Jifunge, kavae viatu vyako. Akafanya
hivyo. Kisha akamwambia, Jivike nguo yako, ukanifuate. Akatoka nje, akamfuata;
wala hakujua ya kuwa ni kweli yaliyofanywa na malaika; bali alidhani kwamba
anaona maono. Na walipopita lindo la kwanza na la pili, wakaja hata mlango wa
chuma wa kuingilia mjini, ukawafungukia wenyewe. Wakatoka nje, wakapita katika
njia moja; mara malaika akamwacha.
Hata Petrao alipopata
fahamu akasema, Sasa nimejua yakini ya kuwa Bwana amempeleka malaika wake na
kunitoa katika mkono wa Herode na katika kutazamia kote kwa taifa la Wayahudi.
Neno la Bwana...
Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 34:1 – 8 (K) 7
(K) Malaika wa Bwana
awaokoa wamchao.
Nitamhimidi Bwana kila
wakati,
Sifa zake kinywani mwangu
daima.
Katika Bwana nafsi yangu
itajisifu,
Wanyenyekevu wasikie
wakafurahi. (K)
Mtukuzeni Bwana pamoja
nami,
Na tuliadhimishe jina
lake pamoja.
Nalimtafuta Bwana
akanijibu,
Akaniponya na hofu zangu
zote. (K)
Wakamwelekea macho
wakatiwa nuru,
Wala nyuso zao hazitaona
haya.
Maskini huyu aliita,
Bwana akasikia,
Akamwokoa na taabu zake
zote. (K)
Malaika wa Bwana hufanya
kituo,
Akiwazungukia wamchao na
kuwaokoa.
Onjeni mwone ya kuwa
Bwana yu mwema,
Heri mtu yule
anayemtumaini. (K)
SOMO 2
2 Tim. 4: 6 – 8, 17 – 18
Mimi sasa namiminiwa, na
wakati wa kufariki kwangu umefika. Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo
nimeumaliza, Imani nimeilinda; baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo
Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu
wote pia waliopenda kufunuliwa kwake.
Lakini Bwana alisimama
pamoja nami akanitia nguvu, ili kwa kazi yangu ule ujumbe utangazwe kwa
utimilifu, hata wasikie Mataifa yote; nami nikaokolewa katika kinywa cha simba.
Bwana ataniokoa na kila neno baya, na kunihifadhi hata nifike ufalme wake wa
mbinguni. Utukufu una Yeye milele na milele. Amina.
SHANGILIO
Mt. 16:18
Aleluya, aleluya,
Wewe ndiwe Petro, na juu
ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu, wala milango ya kuzimu haitalishinda.
Aleluya.
INJILI
Mt. 16 :13-19
Yesu alienda pande za
Kaisaria-Filipi, akawauliza wanafunzi wake akasema, Watu hunena Mwana wa Adamu
kuwa ni nani? Wakasema, Wengine hunena u Yohane Mbatizaji, wengine Eliya,
wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii. Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa
ni nani? Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiye Kristo Mwana wa Mungu aliye
hai. Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na
damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni. Nami nakuambia, Wewe
ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya
kuzimu haitalishinda. Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo
lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote
utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni.
Neno la Bwana... Sifa
kwako Ee Kristo.
Copyright © 2020,
"MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania.
Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment