MASOMO YA MISA,
JUMATANO, JUNI 30, 2021
JUMA LA 13 LA MWAKA
SOMO 1
Mwa. 21:5, 8-20
Ibrahimu alikuwa mtu wa
miaka mia, alipozaliwa mwana wake Isaka. Mtoto akakua, akaachishwa kunyonya;
Ibrahimu akafanya karamu kuu siku ile Isaka alipoachishwa kunyonya. Sara akamwona
yule mwana wa Hajiri Mmisri, ambaye alimzalia Ibrahimu, anafanya dhihaka. Kwa
hiyo akamwambia Ibrahimu, Mfukuze mjakazi huyu na mwanawe, maana mwana wa
mjakazi hatarithi pamoja na mwanangu, Isaka. Na neno hilo lilikuwa baya sana
machoni pa Ibrahimu, kwa ajili ya mwanawe. Mungu akamwambia Ibrahimu, Neno hili
lisiwe baya machoni pako, kwa ajili ya huyo mwana, na huko mjakazi wako. Kila
akuambialo Sara, sikiza sauti yake, kwa maana katika Isaka uzao wako utaitwa.
Naye mwana wa mjakazi nitamfanya kuwa taifa, maana huyu naye ni uzao wako.
Ibrahimu akaamka asubuhi
na mapema akatwaa mkate na kiriba cha maji, akampa Hajiri akimtwika begani
pake, na kijana, akamruhusu; naye akatoka, akapotea katika jangwa la
Beer-sheba. Yale maji yakaishaisha katika kiriba, akamlaza kijana chini ya
kijiti kimoja. Akaenda akakaa akimkabili, mbali i kadiri ya mtupo wa mshale;
maana alisema, Nisimwone kijana akifa; naye akakaa akimkabili, akapazaza sauti
yake, akalia.
Mungu akasikia sauti ya
kijana. Malaika wa Mungu akamwita Hajiri kutoka mbinguni, akamwambia, Una nini,
Hajiri? Usiogope, maana Mungu amesikia sauti ya kijana huko aliko. Ondoka,
ukamwinue kijana, ukamshike mkononi mwako, kwa kuwa nitamfanya kuwa taifa
kubwa. Mungu akamfumbua macho, naye akaona kisima cha maji; akaenda akakijaza
kiriba maji, akamnywesha kijana. Mungu akawa pamoja na huyo kijana, naye
akakua, akakaa katika jangwa, akawa mpiga upinde.
Neno la Bwana...
Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 34 : 6-7, 9-13 (K) 6
(K) Maskini huyu aliita,
Bwana akasikia.
Maskini huyu aliita,
Bwana akasikia,
Akamwokoa na taabu zake
zote.
Malaika wa Bwana hufanya
kituo,
akiwazungukia wamchao na
kuwaokoa. (K)
Mcheni Bwana, enyi
watakatifu wake,
yaani, wamchao hawahitaji
kitu.
Wana-simba hutindikiwa,
huona njaa,
bali wamtafutao Bwana
hawatahitaji kitu
chochote kilicho chema.
(K)
Njoni, enyi wana,
mnisikilize,
nami nitawafundisha
kumcha Bwana.
Ni nani mtu yule
apcndezwaye na uzima,
apendaye siku nyingi
apate kuona mema? (K)
SHANGILIO
Zab. 119:105
Aleluya, aleluya,
Neno lako ni taa ya miguu
yangu,
na mwanga wa njia yangu.
Aleluya.
INJILI
Mt. 8 :28-34
Yesu alipofika ng’ambo
katika nchi ya Wagerasi, watu wawili wenye pepo walikutana naye, wanatoka
makaburini, wakali mno, hata mtu asiweze kuipitia njia ile. Na tazama, wakapiga
kelele, wakisema, Tuna nini nawe, Mwana wa Mungu? Je! Umekuja Kututesa kabla ya
muhula wetu?
Basi, kulikuwako mbali
nao kundi la nguruwe wengi wakilisha. Wale pepo wakamsihi, wakisema, Ukitutoa,
tuache twende, tukaingie katika lile kundi la nguruwe. Akawaambia, Nendeni.
Wakatoka, wakaingia katika nguruwe; na kumbe! kundi lote wakatelemka kwa kasi
gengeni hata baharini, wakafa majini. Lakini wachungaji walikimbia, wakaenda
zao mjini, wakazieneza habari zote, na habari za wale wenye pepo pia. Na
tazama, mji wote ukatoka kwenda kumlaki Yesu; nao walipomwona, walimsihi
aondoke mipakani mwao.
Injili ya
Bwana........Sifa kwako Ee Kristo
Copyright © 2020,
"MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora –
Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see
www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment