MASOMO YA MISA,
JUMAMSI JULAI 3, 2021
JUMA LA 13 LA MWAKA
SIKUKUU YA MTAKATIFU
TOMA, MTUME
SOMO 1
Efe. 2:19-22
Tangu sasa ninyi si
wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa
nyumbani mwake Mungu. Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo
Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni. Katika yeye jengo lote linaungamanishwa
vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika Bwana. Katika yeye ninyi nanyi
mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho.
Neno la Bwana...
Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 117 (K) Mk. 16:15
(K) Enendeni ulimwenguni
mwote, mkaihubiri Injili.
Aleluya.
Enyi mataifa wote,
mhimidini.
enyi watu wote,
mhimidini. (K)
Maana fadhili zake kwetu
sisi ni kuu,
na uaminifu wa Bwana ni
wa milele. (K)
SHANGILIO
Yn. 20 : 29
Aleluya, aleluya, Wewe,
Tomaso, kwa kuwa umeniona, umesadiki, wa heri wale wasioona, wakasadiki.
Aleluya.
INJILI
Yn. 20 :24-29
Mmoja wa wale Thenashara,
Tomaso, aitwaye Pacha, hakuwako pamoja nao alipokuja Yesu Basi wanafunzi
wengine wakamwambia, Tumemwona Bwana. Akawaambia, Mimi nisipoziona mikononi
mwake kovu za misumari, na kutia kidole changu katika mahali pa misumari, na
kutia mkono wangu katika ubavu wake, mimi sisadiki hata kidogo. Basi, baada ya
siku nane, wanafunzi wake walikuwamo ndani tena, na Tomaso pamoja nao. Akaja
Yesu, na milango imefungwa, akasimama katikati, akasema, Amani iwe kwenu. Kisha
akamwambia Tomaso, Lete hapa kidole chako, uitazame mikono yangu; ulete na
mkono wako uutie ubavuni mwangu; wala usiwe asiyeamini, bali aaminiye. Tomaso
akajibu, akamwambia, Bwana wangu na Mungu wangu! Yesu akamwambia, Wewe, kwa
kuwa umeniona, umesadiki; wa heri wale wasioona, wakasadiki.
Injili ya
Bwana........Sifa kwako Ee Kristo
Copyright © 2020,
"MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora –
Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see
www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment