MASOMO YA MISA" MEI
29, 2021
JUMAMOSI
YA 8 YA MWAKA
SOMO
1
YbS.
51:12-20
Wapenzi,
nitamshukuru na kumsifu, na kulihimidi Jina la Bwana. Mimi nilipokuwa kijana,
kabla sijasafiri bado, naliitafuta hekima kwa bidii katika sala yangu, na mbele
ya hekalu nikaomba, nami hata mwisho nitazidi kuitafuta. Ikachanua kama zabibu
inavyoiva, na moyo wangu ukapendezwa, na mguu wangu ukaenda katika njia iliyo
sawa. Tangu ujana wangu nikafanya kuaua, nikaliinamisha sikio kidogo,
nikaipokea, nikajipatia mafundisho tele. Kwangu nira yake ikawa utukufu, nami
nitamshukuru Yeye aliyenifundisha. Kwa maana nalikusudi kujizoeza nayo,
nikajitahidi katika yaliyo mema, wala sitatahayarishwa. Roho yangu imeshindana
kwa nguvu ndani yake, na mintarafu kutenda kwangu nalikuwa mwangalifu;
nikainyosha mikono yangu juu mbinguni, nikaulalamikia ujinga wangu.
Nikaielekeza roho yangu moja kwa moja kwake, na katika unyofu nikaiona; tangu
mwanzo nikajipatia ufahamu, na kwa hiyo sitakataliwa milele.
WIMBO
WA KATI KATI
Zab.
19 : 7-11 (K) 8
(K)
Amri ya Bwana anafurahisha moyo.
Sheria
ya Bwana ni kamilifu,
Huiburudisha
nafsi.
Ushuhuda
wa Bwana ni amini,
Humtia
mjinga hekima. (K)
Maagizo
ya Bwana ni ya adili,
Huufurahisha
moyo.
Amri
ya Bwana ni safi,
Huyatia
macho nuru. (K)
Kicho
cha Bwana ni kitakatifu,
Kinadumu
milele.
Hukumu
za Bwana ni kweli,
Zina
haki kabisa. (K)
Ni
za kutamanika kuliko dhahabu,
Kuliko
wingi wa dhahabu safi.
Nazo
ni tamu kuliko asali,
Kuliko
sega la asali. (K)
SHANGILIO
Zab.
119:18
Aleluya,
aleluya, Unifumbue macho yangu niyatazame, maajabu yatokayo katika sheria yako.
Aleluya.
INJILI
Mk.
11:27-33
Yesu
na wanafunzi walifika Yerusalemu; alipokuwa akitembea hekaluni, walimwendea
wakuu wa makuhani, na waandishi, na wazee, wakamwambia, Ni kwa mamlaka gani
unatenda mambo haya? naye ni nani aliyekupa mamlaka hii uyatende haya? Yesu
akawaambia, Nitawauliza neno moja, nanyi mnijibu, kisha nitawaambia ni kwa
mamlaka gani nayatenda haya. Ubatizo wa Yohane ulitoka mbinguni, au kwa
wanadamu? Nijibuni.
Wakasemezana
wao kwa wao, wakisema, Kama tukisema, Ulitoka mbinguni, atasema, Mbona, basi,
hamkumwamini? Ila tukisema, Ulitoka kwa wanadamu. Waliogopa watu; maana watu
wote walimwona Yohane kuwa nabii halisi. Wakamjibu Yesu, wakasema, Hatujui.
Yesu akawaambia, Wala mimi siwaambii ninyi ni kwa mamlaka gani nayatenda haya.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment