ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Jumamosi,
Mei, 29, 2021,
Juma
la 8 la Mwaka wa Kanisa
YbS
51:12-20;
Zab
19: 8-11;
Mk
11: 27-33
KUMUONA
MUNGU KATIKA MAISHA YETU!
Yesu
sasa yupo Yerusalemu. Katika Injili ya leo, wakati Yesu akiwa anatembea
hekaluni, walimuendea viongozi na wazee Wawayahudi, Makuhani, walimu wa sheria
na Wazee. “nikwa mamlaka ya nani unatenda haya?” walimuuliza Yesu. Hii
ikimaanisha kwamba hafanyi katika hali ambayo inaonesha kujali mamlaka yao.
Kama ilivyo ada kwa Yesu, anawauliza swali na wao. Aliuliza kama kazi ya Yohane
Mbatizaji ilitoka kwa wanadamu au kwa Mungu.
Wakatambua
mara moja kujibu Swahili la Yesu ingewaletea matatizo. Kwa udhaifu mkubwa
wanajibu, “hatujui”. Jibu lisilo lakawaida kabisa tena lisiloridhisha na ajabu
kabisa tena kutoka kwa viongozi wakubwa wa kiroho wa watu. Hapo Yesu akakataa
kuwajibu swali lao walilokuwa wameuliza awali. Hali ya Yesu inafanana na ile ya
Yohane Mbatizaji. Watu waliomsikia Yesu akiongea (“hakuna aliyewahi kuzungumza
namna hii”) na kuona anavyoponya watu (“Mungu amewajia watu wake”), hawakuwa na
wasiwasi wowote juu ya mamlaka yake. “Watu walishangazwa na mafundisho yake,
kwani alifundisha kwa mamlaka sio kama Walimu wa sheria” (Mk 1:22). Swali la
viongozi wa Wayahudi ilidhirisha kabisa udhaifu wao na upofu wao kwenye jambo
ambalo lipo wazi lisiloweza kufichika machoni pa watu wote.
Sisi
pia tunaweza kuwa na upofu huo. Tunaweza tukakataa kuona uwepo wa kazi ya Mungu
katika hali ambazo sisi wenyewe hatutaki kuona, katika watu ambao hatutaki
kuwaona, au kuwadharau baadhi ya watu na kuwaona kama hawana chochote chakuweza
kuniambia pengine kwasababu ya elimu yao au udhaifu wao. Lakini tutambue Mungu
anaweza kumtumia mtu yeyote, jambo lolote, zuri au lisiloonekana zuri machoni
petu, ili kuleta ujumbe wake.
Sala:
Nisaidiye Bwana, kukutafuta na kukupata na nitende yale yote unayotaka nitende
katika Maisha yangu. Amina
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment