MASOMO YA MISA Mei 24, 2021
JUMATATU, JUMA LA 8 LA
MWAKA WA KANISA
SOMO 1
YbS. 17 : 24-29
Hata hivyo huwajalia wale
watubuo kurudi, na wao wanaopotewa na saburi kuwafariji. Basi umrudie Bwana na
kuacha dhambi; omba dua yako mbele za uso wake na kupunguza kikwazo; umgeukie
tena Yeye Aliye juu, uyageue maovu, uyakirihi yaliyo machukizo. Yaani, Mungu
anayo ridhaa gani kwao wanaopotea? ila kwao wanaoishi na kumtolea shukrani.
Shukrani hukoma kutoka kwa wafu, kama kutoka kwake yeye asiyekuwapo; bali
mwenye uzima na afya atamhimidi Bwana, Ee ajabu ya wingi wa rehema za Bwana, na
ya masamaha yake kwao wanaomgeukia!
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 12 :1-2,5-7 (K) 11
(K) Mfurahieni Bwana,
shangilieni, enyi wenye haki.
Heri aliyesamehewa
dhambi,
Na kusitiriwa makosa
yake.
Heri Bwana asiyemhesabia
upotovu.
Ambaye rohoni mwake hamna
hila. (K)
Nalikujulisha dhambi
yangu,
Wala sikuuficha upotovu
wangu.
Nalisema, Nitayakiri
maasi yangu kwa Bwana,
Nawe ukanisamehe upotovu
wa dhambi yangu. (K)
Kwa hiyo kila mtu mtauwa
Akuombe wakati
unapopatikana.
Hakika maji makuu
yafurikapo,
Hayatamfikia yeye.
Ndiwe sitara yangu,
utanihifadhi na mateso,
utanizungusha nyimbo za
wokovu. (K)
SHANGILIO
Zab. 147:12,15
Aleluya, aleluya,
Msifu Bwana, ee
Yerusalemu, huipeleka amri yake juu ya nchi. Aleluya.
INJILI
Mk. 10:17-27
Yesu alipokuwa akitoka
kwenda njiani, mtu mmoja akaja mbio, akampigia magoti, akamwuliza, Mwalimu
mwema, nifanye nini nipate kuurithi uzima wa milele? Yesu akamwambia, Kwa nini
kuniita mwema? Hakuna aliye mwema ila mmoja, ndiye Mungu. Wazijua amri, Usiue,
Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo, Usidanganye, Waheshimu baba yako na mama
yako. Akamwambia, Mwalimu, haya yote nimeyashika tangu utoto wangu. Yesu
akamkazia macho, akampenda, akamwambia, Umepungukiwa na neno moja, Enenda
ukauze ulivyo navyo vyote. Uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni;
kisha njoo unifuate. Walakini yeye akakunja uso kwa neno hilo, akaenda zake kwa
huzuni; kwa sababu alikuwa na mali nyingi.
Yesu akatazama kotekote,
akawaambia wanafunzi wake, Jinsi itakavyokuwa shida wenye mali kuingia katika
ufalme wa Mungu! Wanafunzi wakashangaa kwa maneno yake. Yesu akajibu tena,
akawaambia, Watoto, jinsi ilivyo shida wenye kutegemea mali kuingia katika
ufalme wa Mungu! Ni rahisi ngamia kupenya katika tundu la sindano kuliko tajiri
kuingia katika ufalme wa Mungu, Nao wakashangaa mno, wakimwambia, Ni nani,
basi, awezaye kuokoka? Yesu akawakazia macho, akasema, Kwa wanadamu
haiwezekani, bali kwa Mungu sivyo; maanayoteyawezekana kwa Mungu.
Neno la Bwana... Sifa
kwako Ee Kristo.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment