“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Jumatatu, Mei 24, 2021.
Juma la 8 la Mwaka wa
Kanisa
YbS 17: 20-24;
Zab 32: 1-2, 5-7;
Mk 10: 17-27
KUJIBU WITO WA YESU!
Karibuni sana ndugu
wapendwa kwa adhimisho la Misa Takatifu asubuhi ya leo. Leo neno la Bwana
katika somo la kwanza linatueleza juu ya kumrudia Mwenyezi Mungu, hakika ipo
raha kubwa katika kumrudia Mwenyezi Mungu, kwa sababu wanaomsifu Mungu ni sisi,
na ni kwa wakati huu ndio tunapopaswa kumsifu huyu Mwenyezi Mungu. Huu ndio
wakati pia wa kumrudia, hakuna wakati mwingine, ni wakati tukiwa vijana, tukiwa
na afya tumsifu Mwenyezi Mungu.
Na katika Zaburi yetu ya
wimbo wa katikati, mzaburi anatueleza kwamba ana heri yule aliyesamehewa kosa
na Mwenyezi Mungu. Sisi tukazane, tuungame makosa yetu ili tupate kuionja hii
furaha, dhambi hutufanya tupoteze muda na rasilimali zetu kwa mambo ambayo kwa
hakika hayatupatii msaada wowote. Dhambi hukwamisha mpango wa Mungu alionao
kuhusu maisha yetu. sisi tuziungame dhambi zetu na hakika tutaweza kuionja
furaha zaidi.
Katika somo la injili,
tunakutana na kijana anayeshindwa kuwa mkamilifu kwa sababu ya mali zake.
Anaalikwa kuwa mkamilifu lakini kwa sababu ya kuzipenda mali zake, mali
zilimzuia. Sisi ndugu zangu tujifunze kutambua hatari iliyopo katika
kungangania kitu. Hakika tukiwa watu wa kungangania, hatutaweza kuingia katika
ufalme wa Mungu.
Tuhakikishe hatunganganii
chochote, hata kama ni rafiki au mali hakika tusimnganganie na kushindwa kuuona
ufalme wa Mungu.
Baadhi yetu tumekubali
kungangania marafiki hata wakatuharibu na kuwa watenda dhambi. Tupo tayari
kusema kwamba afadhali niende motoni kuliko kumwacha huyu rafiki. Sisi
tusifanye hivyo, ni lazima tuwe tayari kuachia kwa ajili ya ufalme wa Mungu.
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment