MASOMO YA MISA, MEI 17,
2021
JUMATATU, JUMA LA 7 LA
PASAKA
SOMO 1
Mdo. 19:1-8
Ikawa, Apolo alipokuwa
Korintho, Paulo, akiisha kupita kati ya nchi za juu, akafika Efeso; akakutana
na wanafunzi kadha wa kadha huko; akawauliza, Je! mlipokea Roho Mtakatifu
mlipoamini? Wakamjibu, La, hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia.
Akawauliza, basi mlibatizwa kwa ubatizo gani? Wakasema, kwa ubatizo wa Yohane.
Paulo akasema, Yohane alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini
yeye atakayekuja nyuma yake, yaani, Yesu.
Waliposikia haya
wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu. Na Paulo, alipokwisha kuweka mikono yake
juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao; wakaanza kunena kwa lugha, na kutabiri.
Na jumla yao walipata wanaume kumi na wawili. Akaingia ndani ya sinagogi,
akanena kwa ushujaa kwa muda wa miezi mitatu, akahojiana na watu, na kuwavuta
katika mambo ya ufalme wa Mungu.
Neno la Bwana...
Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATI KATI
Zab. 68 :1-6 (K) 32
(K) Enyi falme za dunia,
mwimbieni Mungu. au: Aleluya.
Mungu huondoka, adui zake
wakatawanyika,
Nao wamchukiao huukimbia
uso wake.
Kama moshi
upeperushwavyo,
Ndivyo uwapeperushavyo
wao;
Kama nta iyeyukavyo mbele
ya moto,
Ndivyo waovu wapoteavyo
usoni pa Mungu. (K)
Bali wenye haki hufurahi,
Na kuushangilia uso wa
Mungu,
Naam, hupiga kelele kwa
furaha.
Mwimbieni Mungu, lisifuni
jina lake,
Shangilieni mbele zake.
(K)
Baba wa yatima na mwamuzi
wa wajane,
Mungu katika kao lake
takatifu.
Mungu huwakalisha wapweke
nyumbani;
Huwatoa wafungwa wakae
hali ya kufanikiwa;
Bali wakaidi hukaa katika
nchi kavu. (K)
SHANG1LIO
Mt. 28 :19, 20
Aleluya, aleluya,
Enendeni, mkawafanye
mataifa yote kuwa wanafunzi, mimi nipo pamoja nanyi sikuzote, hata ukamilifu wa
dahari.
Aleluya.
INJILI
Yn. 16:29-33
Wanafunzi walimwambia
Yesu: Tazama, sasa wasema waziwazi, wala huneni mithali yo yote. Sasa tumejua
ya kuwa wewe wafahamu mambo yote wala huna haja ya mtu akuulize; kwa hiyo
twasadiki ya kwamba ulitoka kwa Mungu.
Yesu akawajibu, Je!
mnasadiki sasa? Tazama. saa yaja, naam, imekwisha kuja ambapo mtatawanyika kila
mmoja kwao kwao, na kuniacha mimi peke yangu; walakini mimi si peke yangu, kwa
kuwa Baba yupo pamoja nami. Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu.
Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.
Neno la Bwana... Sifa
kwako Ee Kristo.
-------------------------
Copyright © 2020,
"MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora –
Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment